MATIKO MWANAMKE ANAYETHUBUTU.
MATIKO MWANAMKE ANAYETHUBUTU.
Tarime
HATUA ambayo Taifa letu limefikia kuhakikisha sharia inayoyatambua
makundi maalu,wanawake,walemavu na Vijana ili kujitokeza kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi inatekelezeka ni nzuri.
Kufuatia sheria hiyo kupewa msukomo na serikali na jamii
kupatiwa elimu na mashirika mbalimbali yakiwemo yasiyokuwa yaserikali
kuwa wanawake,walemavu na Vijana wanayo haki sawa kwa jamii na wanawajibu wa
kuwa viongozi baadhi ya watu kutoka makundi hayo wamejitokeza kuchukua fomu
katika vyama vyao ili kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Hali hiyo imedhihirika kuwa jamii ya Kiafrika kwa sasa hatua
iliyofikia ni nzuri kwa kutoa nafasi ya kuruhusu makundi hayo bila kikwazo
kuchukua fomu na kurusha karata ya kinyang'anyiro cha kuchaguliwa na kuwa
kiongozi.
Katika Wilaya Tarime na vitongoji vyake sharia hii imewapa nafasi
baadhi ya wanawake,vijana na walemavu kujitokeza kugombea baada ya vyama
wanavyotoka kuwapa ridhaa ya kuchukua fomu.
Aidha katika Wilaya Tarime mwanamke pekee ambaye ameonye
ujasiri wa kujaza fomu ili kingia katika mchakato wa kura za maoni hatimaye
kugombea Uongozi ngazi ya Ubunge ni Esther Matiko ambaye ni Mbunge viti maalumu
Mara kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Matiko amesema atakuwa mwanamke wa
kwanza kutoka upinzani ambaye atachukua fomu ykuomba ridhaa kutoka ndani ya
chama chake ili kumpitisha na kugombea nafasi ya Ubunge uchuana na upande wa
pili CCM kwa yeyote watakaye mleta.
Aidha wengine ambao wanatajwa kuwa atchukua fomu na kurusha karata
katika nafasi ya kugombea Ubunge katika jimbo mojawapo baada ya kugawanywa na
kuwa majimbo ya uchaguzi ni Chirstopha Kangoye wa Chama cha
mapinduzi.
Wengine wanaotajwa katika kujarbu karata katika nafasi hiyo ni John
Heche kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Peter
Busene(CHADEMA)Mbunge wa sasa Nyambari Nyangwine wa CCM Michael Kembaki wa CCM
Johanes Manko CHADEMA na Charles Mwera wa CUF.
Licha ya kuwa majimbo yamegawanywa kutoka jimbno moja la uchaguzi
na kuwa majimbo mawili Mbunge Matiko ameonyesha kuwa na umahiri mkubwa
kisiasa huku akifuatiwa na Kangoye kwa sababu ya michango anayoendelea kuitoa
ndani ya jamii ya Tarime bila itikadi hali ambayo imemjenga na kumpa
umaarufu wa kisiasa.
Kwa hatua nyingine mtia nia wa kugombea Ubunge Chirstopha Kangoye
wa Chama cha mapinduzi CCM amejijenga kisiasa huku
wananchi wa Tarime wakidai kuwa wanahitaji Mtu kama huyo ambaye
anatoa misaada kwa wananchi na kuwapunguzia ukali wa garama za michango
mbalimbali inayowasibu.
Kangoye amewahi kutoa misaada ya vitanda kwa wagonjwa katika
hospitali ya Tarime mkoani Mara na kupunguza uhaba uliokuwepo na wagonjwa
kupata mahali pazuri pa kulala wakati wakiwa hospitalini hapo kutibiwa.
Kwa hali hiyo mafahari hao wawili
Kangoye wa CCM na Matiko wa CHADEMA jamii imetokea kuwaamini huku wakisubiri
vyama vyao kuwachagua na kuwapitisha ili kuingia katika mchakato kinyang'anyiro
cha kupambana na wengine ambayo watakuwa wameomba kuygombea nafasi hiyo.
Esther Matiko amesema kuwa kama
chama chake kikimpitisha atahakikisha anaungana na wananchi wa Tarime kuwaletea
maendeleo bila kujali itikadi ya vyama.
Matiko ameonyesha mwanga wa maendeleo katika jamii na kuwatia nia
wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na
kuondokana na dhana potofu kuwa mwanamke hawezi.
Kwa upande wake Rebeka Mjema kutoka shirika
lisilo la kiserikali TGNP wakati wa semina moja ilyofanyika mwaka jana
mjini Morogoro alisema kuwa jamii ikielimishwa na kuondoka na fikira
mgando zinazo tokana na mifumo mibovu ya kiutawala pamoja na mila potofu
watafikia lengo asimia 50 kwa 50 katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika
mwaka huu Okotbar 2015.
Aidha Mjema aliongeza
kuwa waandishi wahabari wanayo nafasi ya kutumia kalamu zao kuelimisha jamii
kuondokana na thana potofu ya kiubaguzi inayofanywa na jamii kukuza makundi
hayo kujitokeza kushiriki kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Mjema alisema kuwa
tamko la umoja wa mataifa la haki za binadamu UDHR(1948) na ICCPR(1978)Ushiriki
kama haki umeainishwa kuwa ni kushiriki katika maswala yote ya jamii moja kwa
moja au kwa kupitia wawakilishi kuchagua na kuchaguliwa katika chaguzi.
Jambo jingine sheria ya
vyama vya Siasa ya mwaka 1992 kifungu cha 8(10(c) inasisitiza uwepo wawanachama
wa jinsia zote na uwakilishi wa makundi yote katika chama.
....................................................................mwisho,,,,,,,,,,,,,,