Matiko atoa msaada wa mabati kwa ajili ya ujenzi wa shule ya awali.
Picha ya Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Mara CHADEMA Esther Matiko akikabidhi Bati 38 kwa wananchi wa Mtaa wa Kogete kata ya Kenyamanyori kwa ajili ya ujenzi wa shule ya awali.
Tarime.
Tarime.
Matiko atoa msaada wa mabati kwa
ajili ya ujenzi wa shule ya awali.
Mbunge wa viti
maalumu mkoa wa Mara CHADEMA Esther Matiko ametoa msaada wa mabati38 katika
mtaa wa Kogete kata Kenyamanyori kwa ajili ya ujenzi wa shule ya awali ili
kuweza kumaliza changamoto inayowakabili wakazi wa mtaa huo kwani walidai kuwa
watoto wao wanateseka kwa kutembea umbali mrefu kufuata Elimu huku wengine
wakijiifadhi katika jengola mtu binafsi ili kupata elimu suala ambalo ni
chanangamoto kwao.
Akikabidhi
msaada huo Mbunge alisema kuwa hiyo ilikuwa ni moja kati ya ahadi aliyoahidi
hapo awali na ameam,ua kufanya hivyo kwa sababu anajua chanagamoto zinzokumba
sekta ya Elimu.
“Mimi
nisesomea katika mazingira magumu hivyo
kama mbunge wenu japokuwa sina mfuko wa jimbo najipigapiga mshahara wangu na
posho ili kuweza klupunguza baadhi ya changamoyo ikiwemo suala zimza la Elimu”
alisema Mbunge.
Aidha mbunge
aliongeza kuwa kwa kuwa jingo hilo linamahitajiya mabati50 hivyo yaliyobaki aliweza kutoa ahadi nakusema
kuwa ataweza kuwapatia mabati hayo ili waweze kujenga jingo hilo huku
akiwaimiza wananchi kujitolea ili jingo hilo la awali liwezekukanmilika mapema
ili watoto waweze kupata haki ya ya Msingi ya kielimu.
Aniseth
Magabe ni mwenyekiti wa mtaa wa kogete
alisema kuwa baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kufanyika na kogete kuwa mtaa
mpya nakata mpya ya Kenyamanyori mtaa wake serikali imeusahau suala ambalo
linazidi kumpa changam,oto ili kuweza kuwaletea wananchi wake maendeleo.
“Kabla ya
mtaa kugawanyika wanafunzi walikuwa na shule lakini badae ilibomoka hivyo kwa
sasa tumejipanga na wananchi kuweza kujenga shule mpya ya awali tunatoa
shukranizetu kwambunge wetu ambaye ameweza kusikiliza kilio chetu sisi
wanakogete” alisema Magabe.
Magabe
aliongeza kuwa juhudi zake kwakushirikiana na viongozi wake pia wameisha weka
tiripu moja yam awe ili kuoneshja juhudi walizonazo kwa lengo la kusukukma
maendeleo katika mtaa huo.
Hata hivyo
wananchi hao waliweza kutoa kiliochao kwa mbunge huyokuwa ni sula zima la maji
suala amblo linapelekea wananchi hao wazidi kutumia visima vya asili ambavyo
siyo salama kwa afya zao .
“Maji
yanaenda mjini yanatoka katika mtaa huu l;akini sisi wananchi wa kogete hatuna
maji ya bomba tunaomba kilio chetu kisikilizwe” walisema wananchi hao.
……Mwisho….