ACACIA WAKABIDHI VISIMA 38 VYENYE THAMANI YA SHILINGI BILLIONI MBILI NA NUSU.

Picha ya Afisa Elimu Msingi (W) Tarime Emmanuel Johnson kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Athuman Akalama akitwisha ndoo ya maji mmoja wa  wa wananchi wa kijiji cha Nyamwaga baada ya kuzindua Mradi wa Maji ambao umetengenezwa na kampuni ya uchimbaji wa dhahabu ACACIA Uliopo Nyamongo.
                                                      Tarime.
ACACIA WAKABIDHI VISIMA 38 VYENYE THAMANI YA SHILINGI BILLIONI MBILI NA NUSU.

Mgodi wa uchimbaji wa Dhahabu ACACIA Norh Mara uliopo Nyamongo Wilayani Tarime Mkoani Mara Umekabidhi Visima 38 vikiwemo visima virefu na vya bomba vyenye thamani ya shilingi Billioni Mbili na Nusu  katika vijiji 11 vinavyozunguka Mgodi huo kwa lengo la kuondolea changamoto ya Upatikanaji  wa Maji ikiwa ni pamoja na kupunguza umbali mrefu kwa wananchi hao ambao wamekuwa wakitembea kufuata huduma ya maji ili kuweza kukidhi mahitaji yao huku wakiboresha  mahusiano Mema baina ya Wananchi na Mgodi huo.


Akiongea na Wananchi Afisa mahusiano  kutoka katika mgodi wa Acacia  Zakayo Karebo amesema kuwa Mgodi huo umekuwa ukitekeleza miradi ya jamii  kulingana na sera ya mgodi huo ikiwemo huduma ya Afya Maji na Elimu kwani vitu hivyo ni muhimu sana kwa mwanandamu
Afisa mahusiano amesema kuwa faida inayopatikana na uzalishaji huo inapaswa kutekeleza miradi mbalimbali ya jamii kwa lengo la kuboresha mahusiano baina ya  Mgodi huo ili kuweza kuwaondolea utegemezi wananchi ho kupitia vijiji vyote vinavyozunguka mgodi huo.


Mgodi huo umeweza kuchimba Visima 54 sawa na asilimia 70  huku vilivyofanyakazi ni visima 38 ambapo vimetumia shilingi Billion Mbili na Nusu fedha za kitanzania
Kwa niaba ya Meneja wa Mgodi huo Mr Garry Chap Man Walter Grigory amesema kuwa Maji ni uhai na mgodi umewekeza fedha za kutosha katika kutekeleza miradi hiyo kwa wananchi   hivyo ametoa rai kwa wananchi kutunza miradi hiyo kwa ajili ya kzazi kijacho.

Emmanuel Jonson ni Afisa Elimu Msingi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Athumani Akalama akikabidhiwa miradi hiyo ya Maji amesema kuwa  jamii iondokane na dhana ya kuwa  miradi ni  mali ya wafadhili huku akiutaka uongozi wa serikali za vijiji na kamati za maji kutunza visima hivyo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kwa ujumla

 Akisoma risala kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Kerende mtendaji wa kijiji charles Kizito amebainisha changamoto  kuwa Visima bado ni vidogo kulingana na mahitaji ya wananchi hivyo alitumia fursa hiyo kuomba mgodi huo kuongeza visima vya kutosha huku akitoa ushauri kuwa Uongozi wa mgodi kwa kushirikiana naHalmashauri ya Wilaya ya Tarime  wajenge mazoea ya kutembelea visima hivyo mara kwa mara huku wakibaini changamoto na kuzifanyia kazi mara moja.
Powered by Blogger.