Matiko atoa msaada wa Mifuko 60 saruji na bando mbili za mabati kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi Tarime.
Picha ya Mratibu wa Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Mara Leonard Nyankang'a katikati aliyevaa kofia akikabidhi mifuko20 ya saruji iliyotolewa na M,bunge wa Viti maalumu Mkoa wa Mara Ester Matiko kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mosege Kata ya Nyarukoba Wilayani Tarime.
Matiko atoa msaada wa Mifuko 60 saruji na bando mbili za mabati kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi Tarime.
Matiko atoa msaada wa Mifuko 60 saruji na bando mbili za mabati kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi Tarime.
Mbunge wa viti malumu kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Mkoa wa Mara Ester Matiko ametoa msaad wa Mabati bando Mbili na Mifuko 60 ya
saruji kwa ajili ya kuunga wananchi mkono kutokana na juhudi walizonzo katika
ujenzi wa Maabara, Zahanati na Ofisi za serikali za vijiji ambabyo kwa sasa
vinajengwa kwa nguu za Wananchi.
Akikabidhi Vifaa hivyo kwa niaba ya Mbunge Leonard Nyankang'a alisema kuwa
wanaendela kutimiza ahadi za mbunge ambazo alitoa baada ya wiki tatu zilizopita
kipindi alipokuwa akizungukia majimbo ili kubani changamoto za wananchi
walizonzo.
"Tuliweza kupita na mbunge na kubaini changamoto za wananchi na mbunge
wetu akaweza kutoa ahadi za saruji pamoja na saruji hivyo leo tumeamua
kukabidhi vigfaa hivyo kwa wananchi" alisema Nyankang'a.
Mratibu huo wa Mbunge amekabidhi mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa
Zahanati ya kijiji cha Mosege kata Nyarukoba, Mifuko 20 ya saruji shule ya Sekondari Gibaso kwa ajli
ya ujenzi wa Maabara, Bando Moja ya bati
kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya kijiji Karagatonga, Mifuko20 ya saruji
na bando moja ya bati kwa jili ya ujenzi wa shule ya Msingi Nyabirongo ambayo
inajengwa kwa nguvu za wanananchi ili kuokoa mwendo mrefu ambao wanafunzi
wanafuata huduma ya masomo mbali.
Akipokea misaada hiyo Diwani wa kata ya Nyarukoba kupitia tiketi ya Chadema
Mstafa Msian alisema kuwa kutolewa kwa misaada hiyo kunaonesha jinsi viongozi
wa chadema walivyo na moyo wa kusaidia.
"Mbunge wetu hana mfuko wa jimbo lakini anajinyima kutokana na
mshahara wake ansaidia wananchi wake ni jambo la kujivunia sisi kama viongozi
wa Chadema" alisema Msiani.
Kw upande wake Mbunge wa viti maalumu Ester Matiko alisema kuwa ni wajibuy
wke kutoa misaada kwa wananchi pale wanapoonesha juhui za kutaka kuleta
maendeleo.
"Natumia mshahara wangu kusaidia wananchi wangu pia mimi nina majukumu
ya kusaidia Mkoa Mzima ambao uko na majimbo mengi lakini wananchi wangu
wakinipa ridhaa ya kuongoza nikapata mfuko wa jimbonitaweza kufanya makubwa
zaidi ya hayo" alisema Matiko.
....Mwisho...