487 waitimu chuo cha ualimu ngazi ya Cheti
Picha ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorius Luoga akiongea na wanachuo Chuo cha Ualimu TTC Tarime hawapo pichani katika mahafari ya 23.
CHUO
cha ualimu TTC Tarime Mkoani Mara wananchuo 487 wameitimu mafunzo ya
ualimu daraja la (111)A, katika mahafari hayo ya 23 mgeni rasmi alikuwa
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Glorius Luoga.
Katika
mahafari hao Mmoja wa wananchuo Devotha Mangarila akisoma risala
alizitaja chanamoto zinazokumba chuo hicho huku wadau wote wa maendeleo
kutoka nje na ndani kujitokeza kwa wingi kutoa michango yao ili
kusaidia na kuboresha miundo mbinu na wanachuo kupata mahali pazuri pa
kujisomea.
Akisoma
risala kwa mgeni rasimu mkuu wa wilaya Tarime Glorius Luoga mkuu wa
chuo hicho Nicholaus Magige alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo uhaba wa maji,uchakavu wa majengo,ukosefu wa
maabara,ukosefu wa maktaba,upungufu na uhaba wa nyumba za watumishi hali
ambayo inasabisha kuwa na kilio cha mda mrefu bila msaada.
Aidha Magige
alisema kukubali kuwa mgeni rasimi wa maafali ya 23 ya chuo cha ualimu
Tarime mkoani Mara utakuwa suluhisho la kilio cha mda mrefu ambacho
kimekuwa kikitolewa na chuo hicho kwa kila mgeni ambaye anakuja
kutembelea chuo hicho.
Sanjari
na changamoto hizo Magige alisemakuwa chuo hicho wahitimu wa mwaka wa
pili daraja la tatu A, walisasjiliwa 2013 wakiwa 503 ambapo wanaohitimu
ni wanachuo 487 huku 16 hawakuhitimu kwasababu mbalimbali ikiwemo kihama
na kifo.
Naye
mkuu wa wilaya Tarime Luoga alisema kuwa atahakikisha wanaanda mkakati
wa kuvuna maji hapo chuoni na kuondoa kero iliyopo ya maji kwanza huku
kero zingine zilizobaki zikiendelea kutafutiwa uvumbuzi.
‘Nitahakikisha
chuo kinakuwa na sehemu ya kuvunia maji na kupata maji ya uhakika na
kupuinguza kero iliyiopo kama sio kumaliza kabisa’’alisema Luoga.
Aidha
Luoga aliwataka wahitimu kuepuka kujiunga katika makundi ya wanasiasa
badala yake watumiwe mda uliobaki kukamilisha kujisomea na kupanga
mipango ya maisha kwa kuzingatia kuwa jamii na wazazi wanawategemea
kufamnya vizuri nawala sio kuwaangusha.
Hata hivyo mkuu wa wilaya amewaasa waanchua hao kuondokana na taamaa aza maisha pale wanapopata ajili
“Mkisha
ajiliwa wengine munataka mafaniki ya haraka na kuelekea pasipositahili
hebu jaribu kuepukana nahilo kwa lengo la kujiletea maendeleo” alisema
Mkuu wa Wilaya.
Sanjari
na hayo Mkuu wa wilwyw huyo aliongeza kuwa Serikali haina budi kutoa
ajira kwa waitimu hao ambao mwaka huu wameitimu Ngazi ya Cheti kwani
kubadilika kwa mitahara kukmewakuta tayari wanaitimu hawa.
“Mimi
kama mutumishi wa Serikali nashauri Wizara ya Elimu kuangalia jaira kwa
wamnachuo walimal;iza ngazi ya Cheti ili badae wasaidiwe na
kujiendeleza ili kufikia Sitashahada” alisema ,.