Ubalozi wa china wakabidhi maabara katika shule ya Msingi aliyosoma Baba Taifa.
Picha ya Balozi wa China Dr Lu Youqing kulia wa kwanza akikata utepe katika uzinduzi wa Maabara ya kisasa iliyojengwa na ubalozi wa china katika shule ya Msingi Mwisenge ambapo alisoma Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Aseri Msangi akifuatiwa Meya wa Manispaaya Musoma Alex Kisurura
Ubalozi wa china wakabidhi maabara katika shule ya Msingi
aliyosoma Baba Taifa.
Ikiwa rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Murisho kikweteanatilia mkazo ujenzi wa maabara
tatu kwa kila shule za Sekondari hapa Nchi kwa lengo la kuongeza ufauru mkubwa katika
masomo hayo,Ubalozi wa China kupitia
balozi wake Dr Lu Youqing wamekabadhi Maabara moja katika shule ya Msingi Mwisenge
iliyopo manispaa ya Musoma ambayo ni moja ya Shule aliyesoma Baba wa
Taifa Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere kwa lengo la kuchochea masomo ya
sayansi kwa watoto wa shule za msingi kusoma masomo hayo kwa vitendoikiwa ni
pamoaj na kuenzi Baba wa Taifa.
Akikabidhi maabara
hiyo Balozi wa China amesema kuwa maabara hiyo imejengwa kwa lengo la kumuenzi
wa wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere
katika uhai wake kwani alichangia kwa kiasai kikubwa kuleta mahusiano
mema baina ya Nchi ya Tanzania na ubalozoi
wa China huku akisema kuwa Mwl Nyerere alikuwa Mwanasiasa wa kueshiiwa na
Mwanzilishi wa ukombozi wa Bara la Afrika.
“Mwalimu Nyerere
alikuwarafikimzuri wa China pamoja na Mwenyekiti Mao Zedong, Waziri Mkuu Zhou
Enlai na Viongozi wengine wa China wao waliweza kupanda mbegu ya Urafiki baina
ya Nchi ya Tanzania na Ubalozi wa China” alisema Dr Lu Youqing.
Aliongeza kuwa
Ubalozi wa china umeanza kutoa tuzo kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika
masomo ikiwa ni pamoja na kujenga masomo moja.
“Rais kikwete
anatilia mkazo sana katika masomo ya sayansi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa
maabara ni maamuzi sahihi ya kimkakati katika kukuza Viwanda na kukuza uchumi
wa Taifa la Tanzani” alisema Balozi.
Akisoma Risala mbele
ya Mgeni rasimi Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Mwisenge Elias Makoro aliweza
kutoa historia fupi ya shule hiyo huku akisema kuwa shule hiyo wameweweza kusoma
viongozi wakubwa wakitaifa hivyo aina budi kupewa kipaumbele katika kuiboresha
na kuwa mfano bora katika shule zote zilizomokatika Manispaa ya Musoma Mkoani
Mara.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Aseri
Msangi alisdema kuwa uwepo wa maabara katika Shule ya Msingi Mwisenge itakuwa
chachu kubwa ya kusoma masomo ya sayansi.
“Tunatia shukrani
zetu katika ubalozi wa china uwepo wa Maabara hii itakuwa chachu kubwa ya
watoto wetu kusomA Masomo ya Sayansi” alisema Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Makongoro Nyerere ni
Mbunge wa Afrika Mashariki alisema kuwa mahusiano mazuri na urafiki ulikuwepo
na Hayati Baba wa Taifa na Viongozi wa Balozi wa China umesababisha kujengwa
kwa maabara katika shule ya Msingi ambayo alisoma Julius Kambarage Nyerere.
“Watoto wetu
hawatasahau msaada huu ambao mumeweza kutoa nyie ubalozi wa china” alisema.
Kwa Upande wake meya
wa manispaa ya Musoma Alex Kisurura alitoa shukrani zake kwa ubalozi wa
China kwa niaba wakazi wote wa Musoma
kwa Msaada huo wa ujenzi wa Maabara katika shule ya Msingi kwani ni Shule ya
kwanz Mkoani Mara kuwa na Maabara katika shule za Msingi.
Sanjari na hayo
balozi wa china alisema kuwa kuwa mbali na kukabidhi Maabara hiyo ataweza kuleta na vifaa vyake
ili wanafunzi waweze kusoma mara moja kwa vitendo n kuongeza ufauru.
......M wisho...