CHADEMA WAITAKA SERIKALI KUTANGAZA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA SHIRATI,.

Picha ya katibu wa Mkoa CHADEMA Mwl Chacha Heche akikabidhi kitabu cha Mwongozi wa utawala bora kwa wajumbe baada ya kufungua Mafunzo hayo.                                      Rorya.
CHADEMA WAITAKA SERIKALI KUTANGAZA MAMLAKA YA MJI MDOGO WA SHIRATI,.

CHAMA cha Demokrasia na Maendelo CHADEMA kupitia Katibu wake ngazi ya Mkoa Mwl Chacha Heche wameitaka serikali kutangaza Mamlaka ya Mji Mdogo wa Shirati kwa lengo la kuwaletea wananchi Maendele kwani tangia chaguzi za serikali za mitaa kumalizika na Chadema kuongoza  kwa ushindi lakini Serikali imekaa kimya kutangaza Mamlaka ya Mji huo mdogo wa shiriti.
Kauli hiyo imetolea hivi karibuni katika kufungua mafunzo ya viongozi wa chama hicho ngazi ya Kitongoji, Mitaa,Vijiji,kata ambao walichaguliwa katika hauzi za serikali za mitaa.

Katibu aliesema kuwa tangia kumalizika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa na chadema kuongza mitaa katika ushindi bado serikali imekaa kimya na wananchi wanataka maendeleo.

"Chaguzi hizi CCM wangekuwa ameshinda sasa hivi mamlaka ya mji wa shirati ungelikuwa meishatangaza zamani sasa serikali isituelewa ibaya tukifanya maamuzi yeyote kwa sababu tuanataka maendeleo ya wananchi na viongozi wetu wanataka kufanya kazi" alisema Mwalimu Chacha.

Aidha Heche amesema kuwa taratibu na kanuni za mamlaka zipo ambazo Mji wa Shirati uanatoshereza na selikali imekaa kimya huku maendeleo ya wananchi yanakwama.
Charles Odero ni Mwenyekiti wa CHADEMA Wilayani Rorya alisema kuwa katika jimbo la rorya Mji mdogo wa shiratichadema wailishnda vijiji 34 vitongoji 180 na mitaa 7 lkini serikali wamekaa kimya bila ya kutangaza mamlaka ya Mji mdogo wa shirati Wilayani Rorya Mkoani Mara.

"Kama ni kazi ya kuamasisha juu ya chama nilifanya kwa kushirikiana na vingozi wenzangu lakini nashangaa serikali yetu ambayo inaongozwa na Chama cha Mapinduzi"  alisema Odero.

katibu wa Chama hicho Mkoa Mwl Chacha Heche amesema kuwa mafunzo hayo yanafanyika Mkoa Mzima ili kuweza kuwajengea uwezo viongozi wote waliochaguliwa katika serikali za mitaa.
.Mwisho..
Powered by Blogger.