Ester Matiko atao mipira ya Netbali katika Majimbo.

Picha ya Mbunge wa viti maalumu CHADEMA Mkoa wa Mara Ester Matiko akikabidhi mpira kati ya mmoja ya wajumbe kwa jili ya kutoa hamasa hususani Michezo kwa akina Mama.
                                     Musoma.
Mbunge wa viti maalumu kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ester Matiko ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Mkoa wa Mara (BAWACHA) ametoa mipira Minane  katika majimbo pamoja na wilaya zilizomo ndani ya Mkoa wa Mara kwa lengo la kuinua michezo kwa wanawake.

Mbunge huyo alisema kuwa wanawake wamesaulika katika  suala zima la michezo hivyo ametumia fursa hiyo kutoa miira hiyo kwa lengo la kutoa hamasa kwa akina mama ili waweze kupenda michezo.
"Tumekuwa tukitoa misaada ya vifa vya michezo hususani katika timu za mpira wa miguu na wanawake wamesauli kwakuwa mimi ni mchezajai na ninapenda michezo ndo maana nimewiwa kuwapa msaada huo akina  wanawake" alisema mbunge.

Wakipokea msaada huo wanawake ambao ni wajumbe kutoka majimbo na wilaya wlisema kuwa mipira hiyo itakuwa chachu kwa akina mama ambao ni wapenzi wa michezo huku wakiwaomba wafadhili mbalimbali kuwapa vifaa vya michezo akinamama hao.

Mbunge wa viti maalumu CHADEMA Mkoawa Mara Ester Matikoamekuwa akisaidia sana vifaa vya mchezo ikiwa ni pamoja na kufadhili mashindano mbalimbali kwa lengo la kuibua vipajai mbalimbali bna kuviendeleza suala ambalo linawapa hamasa wakazi wa Mkoa wa Mara ikiwemo wilaya ya Tarime.


                              .....MWISHO...
Powered by Blogger.