BODABODA WACHANGUA UONGOZI NGAZI WILAYA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Picha ya Mwenyekiti aliyechaguliwa wakwanza kutoka kushoto akisal;imiana na wajumbe bnaada ya uchaguzi huo.

                                                  Tarime.
BODABODA WACHANGUA UONGOZI NGAZI WILAYA ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI.

WAENDESHA pikipiki maarufu kama bodaboda katika Halmashauri ya wilaya ya Tarime Mkoani Mara wamechagua uongozi ngazi ya Mwenyekiti, Katibu, Mhazini , Mtunza nidhamu, kamanda kwa ajili ya ulinzi na usalama uchaguzi huo humeafanyika kwa lengo la kuwa na umoja pamoja na mshikamano ili kuweza kuondoa  matukio ambayo yamekuewa yakitokea mara kwa mara ussani mauaji ya waendesha pikipiki.

Pia  Uongozi huo utasaidia waendesha pikipiki kuwa na nidhamu ikiwa ni pamoja na kufuata kanuni na sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajili zisizokuwa za lazima.

Kwa upnade wa Mwenyekiti amechaguliwa Marwa Ryyoba Mhechi kura 48  katibu Yusuph Edward kura 31, Mhazini Kisiri Machumbe kura36, Mtunza nidhamu Dan Msimamo kura 22 huku akichaguliwa kamanda wa bodaboda ambaye ni Masiagi Mseti kwa ajili ya kudumisha ulinzi n ausalama kwa waendesha pikipiki hao.

Marwa Ryoba Mhechi ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha waendsha bodaboda ngazi ya wilaya katika Halmashauri ya Mji wa Tarime alisema kuwa umoja na mshikamno ndo chchu ya maendeleo endapo watamupa ushirikiano wa kutosha itasaidia kuwainua na kubadili mitazamo ya wandesha bodaboda.

"Jamii imeisha iwekea mitazamo kuwa isisi boda boda ni wavurugaji naomba tusitumike vibaya na watu wasipenda maendeleo" alisema Mhechi.
Akiongea bada a uchaguzi hu Diwani wa kata ya sabasaba Christopher Chomete alisema kuwa kupitia Halmashauri ya mji wa Tarime watazidi kuwasaidia waendesha boda boda hao kwa lengo la kujikwamua kiuchumi.
"Katika kusaidia uwezi kusadia mtu mmoja mmoja lakini kwa kuwa mmeungana tutajua jinsi ya kuwasaidi hebu endelezeni umoja wenu utaweza kuiwasaidia" alisema chomete.

Sanjari na kufanyika kwa uchaguzi huo chama hicho kinaendelea na kuboresha katiba itakayotmika kuwalinda na kulinda viongozi pamoja na wanachama wote.

                                                                   ....Mwisho...
Powered by Blogger.