BAWACHA WANAWAKE JITOKEZENI KUGOMBEA NYADHIFA ZA UONGOZI.

BAWACHA WANAWAKE JITOKEZENI KUGOMBEA NYADHIFA ZA UONGOZI.

Baraza la wanawake  Mkoa wa Mara  (BAWACHA) limewataka akina mama kujitokeza kwa wingi kugombea nyadhifa mbalimbli za uongozi  kwa lengo la kumkomboa mwanamke ikiwa ni pamoja ana kuondoa dhana potofu ambazo jamii imejenga kuwa  mwanamke hawezi kuongoza.

kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la wanawake Bawacha Mkoa wa Mara Ester Matiko ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara katika kikao kilichojumuisha wajumbe kutoka majimbo pamoja na wilaya zilzzomo katika mkoa wa Mara na kuanyika katika ukumbi wa ofsi ya chadema mjini musoma kwa lengo la kupokea tarifa mbalimbali pamoja na changamotozinazwakabili ili kuweza kuzifanyia kazi.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa wamekutana pia kuweka mikakati kuhusu uchaguzi ulioko mbeleni.

"Tunajua mwanamke ni kiungo muhimu katika chama chetu hivyo hatuana budi ya kuwaandaa wanawake wote ili kuweza kijitokeza kugombea nyadhifa mbalimbali ukiwemo Ubunge na Uraisi kwa lengo la kukomboa mwanamke" alisema Mwenuykiti.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa kuhusu viongozi waliochaguliwa bado wanakumbwa na changamoto mbalimbali hivyo ili kuweza  kuwajengea uwezo mkubwa viongozi hao atatoa mafunzo kwa kila Wilaya pamoja na majimbo yaliyomo ndani ya Mkoa wa Mara.

Angela Derrick   ni Katibu Baraza la Wanawake Musoma Mjini amewashauri akina mama kuanza  kuunda vikundi mbalimbali  ili viweze kusaidiwa kwa lengo la kupunguza umaskini.

"Mbunge ana wajibu wa kusaidia lakini hawezi kuaidia kila mmoja au kikundi kimoja wanawake tukiungana tukaelimishana itasaidia sana ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi midoomidogo ili kuondoa utegemezi tutajikwamua kiuchumi na kisiasa" alisema Angela.


                   ....Mwisho...
Powered by Blogger.