Kembaki amusaidia Mwanamke aliyekatwa mapanga na Mmewe.




Kembaki amusaidia Mwanamke aliyekatwa mapanga na Mmewe.
Mwanamke Anasitazi John miaka 18  aliyeshambuliwa january22 na mme wake aliyejulikana kwa jina la John Weghai katika kata ta Mriba wilayani Tarime Mkoani Mara ataimaye amepata msaada wa fedha za matibabu kwa ajili ya kuokoa maisha yake,
Mama huyo alishambuliwa na mme wake kwa mapanga katika mkono wa kushoto pamoja na titi lake la kushoto kwa kisa cha kuwa hazai na wameweza kukaa katika ndoa yao takribani miaka 3 bila ya kubahatika kupata watoto suala ambalo limekuwa changamoto katika maisha yao.

“Alikuwa akinishambulia kwa vipigo mara kwa mara na ndipo nilamua kwenda nyumbani niliporejea kwangu ndipo aliamua kunifanyia kitendo hicho” alisema Anasaitazia.

Michael Kembaki ni mfanyabihashara pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Memorial Foundation katika jiji nla Arusha ameweza kutoa msaada wa matibabu kwa mama huyo kwa lengo la kuokoa maisha yake, akizungumza na gazeti hili alisema kuwa ameamua kusaidia mama huyo kwa sababu ameguswa sana baada ya kuona mama huyo jinsi alivyofanyiwa vitendo vya ukatili dhidi ya Mmewe kwa kisa cha kutozaa kwani hiyo ni mipango ya mwenyezi mungu.

“Katika maisha yangu nimejaliwa kusaidia jamii yote kwa kile kichache mwenyezi mungu ambacho amenjialia lengo ni kuokoa mama huyu iliaweze kwenda Bugando kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi” alisema Kembaki.

Kembaki alitoa Tsh 200,000 kugarimia nauli na garama ya kumfikisha majeruhi Bugando Mwanza pamoja na Tsh 50,000 kugarimia chakula cha mgonjwa ambaye hana jamaa na ndugu kipindi alipopata nafasi ya kutembelea wagonjwa katika Hospitali ya Halimshauri ya mji wa Tarime kwa lengo la kuwajulia hali, huku akiwapelekea Sabuni, matunda na Mahitaji mengin muhimu ya Binadamu.

 Aidha kembaki alitumia nafasi hiyo kuiomba jamii kuondokana na vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na kumpa mwanamke nafasi kubwa katika jamii huska na si kumunyanyasa, Vipigo vya kila mara  suala ambalo linazidi kumkatisha tama.
                                                           …….Mwisho…
Powered by Blogger.