WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUELIMISHA JAMII KUWAPA NAFASI WANAWAKE,WATU WENYE ULEMAVU NA VIJANA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI.

Picha ya waandishi wa habari kutoka mikoa Nane wakiwa katika semina ya mafunzo katika ukumbi wa usambala lodge Morogorowakijifunza  juu ya uelimishaji kwa akina mama vijana na makundi maalumu kujitokeza katika kugombea nafasi za uongozi katika chaguzi zilizopo mbeleni.



WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUELIMISHA JAMII KUWAPA NAFASI WANAWAKE,WATU WENYE ULEMAVU NA VIJANA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI.

WAANDISHI wa habari wametakiwa kutumia kalamu Zao  kuandika  habari za kuelimisha jamii kuhusu Wanawake,watu wenye ulamavu pamoja na Vijana  kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na mwezeshaji Grace Kiseru wakati akitoa mafunzo ya ushiriki wa Wanawake,Watu wenyeulamavu na Vijana katika uchaguzi ambayo yameandaliwa na Shirika la haki za binadamu LHRC na TGNP yaliyofanyikia ukumbi wa hoteli ya Usambara nanenane.

Grace alisema kuwa waandishi wa habari wanayo nafasi kubwa kuelimisha jamii kuhusu maswala ya uchaguzi hususani Wanawake,watu wenyeulamavu pamoja na Vijana kugombea na kuchaguliwa nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuwa ni haki zao za kimsingi na kikatiba.   

Semina hiyo iliwashirisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mara,Simiyu,Mtwara,Mbeya,Shinyanga,Maorogoro,Ruvuma na Pwani ambayo iliandaliwa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika habari za Wanawake,Watu wenye ulamavu na Vijana ili waweze kujitokeza kushiriki na kugombea nafasi mbalimbali za uchaguzi na kuwa ni haki yao ya kimsingi na kisheria. 

Naye kwa  upande wake Rebeka Mjema ambaye pia ni mwezehaji alisema kuwa jamii ikielimishwa na kuondoka na fikira mgando zinazo tokana na mifumo mibovu ya kiutawala pamoja na mila potofu zinazochangia makundi hayo kutoshirikishwa katika kuchaguliwa na kuwachagua viongozi kwa sababu tu kuwa hawana uwezo Nchi itakuwa na maendeleo.

Aidha Mjema aliongeza kuwa waandishi wahabari wanayo nafasi ya kutumia kalamu zao kuelimisha jamii kuondokana na thana potofu ya kiubaguzi ambayo inanyanyapa makundi hayo na kushindwa kuwadhamini hususani katika maswala ya kushiriki siasa.

                                                  …MWISHO..


Powered by Blogger.