Mwanamke akatwa panga nammewe kisa kushindwa kuzaa watoto

Ni picha ya Anasaitazia John Miaka 18 Mkazi wa kata ya Mriba Wilayani Tarime Mkoani Mara akiwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime  akionesha majeraha katika mkono wa kushoto karibu na titi


Mwanamke akatwa panga nammewe kisa kushindwa kuzaa watoto

WAKATI wa ziara ya aliyekuwa Mke wa Rais wa kwanza Afika kusini Nelson Mandela, Graca Mache ikifanyika katika mkoa wa Mara katika Wilaya Tarime kwa lengo la kuchochea mabadiliko ya jamii ili kuondokana  na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa Mama na mtoto Mkazi wa kata ya Mriba Anastazia John 18 amejeruhiwa na Mme wake wa ndoa kwa kukatwa mapanga mkono wake wa kushoto na sehemu ya titi la kushoto na kumsababishia maumivu makali, kwa kile ambacho kinasemekana kuwa katika ndoa yao hajabahatika kupata mtoto hata mmoja
Tukio hilo lilitokea majira ya saa 1,00 usiku Januari,22 mwaka huu wakati wakiwa nyumbani kwake mriba baada ya kurudi kutoka nyumbani kwao alipokuwa amekimbilia baada ya ugomvi kuzuka baina ya  Mme wake huyo kuwa ameshindwa kumzalia mtoto.
“Mme wangu alianza kunigombeza hap awali na ndipo nilamua kukimbia nyumbani kwa wazazi wetu niliporejea tena ndipo ugomvi ukaanza tena na kunishambulia kwa mapanga sehemu zangu za mkono wa kushoto karibu na titi” alisema Anasaitazia.
Aidha wakati akiwa hospitalini hapo mhanga huyo Dakitari wa zamu Lestuta Kaminda alisema kuwa mgonjwa huyo anahitajika kwenda hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza kwa lengo la kufanyiwa uchunguzi zaidi wa kimatibabu ili kunusuru maisha yake.
Mda mfupi baada ya Daktari kutoa mwito huo alitokea masmaria mwema Machael Kembaki ambayeni mmoja wa wafanya bihashara katika jiji la Arusha pia ni mkazi wa Wilayani Tarime Mkoani Mara ambapo anafanyia kazi Arusha kambapo ni Mkurugenzi wa kampuni ya Memorial Foundation aliweza kutoa msaada wa ghalama zitakzomyibu Anasitazia zikiwemo ghalama za usafiri.  
Kembaki alitoa zaidi ya Tsh 400,000 ikiwa ni pamoja kununua mahitaji ya wagonjwa katika Hospitali ya Halmshauri ya mji wa Tarime kipindi alipoenda kuwapa pole.
“Nimetoa msaada wa shilingi Tsh 200,000 kugarimia nauli na garama ya kumfikisha majeruhi Bugando Mwanza pamoja na Tsh 50,000 kugarimia chakula cha mgonjwa ambaye hana jamaa aliyelazwa katika hospitali ya Bomani”alisema kembaki.
Aidha Michel alisema kuwa kufanyika kwa vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto wa kike ni kumfanya asitimize ndoto zake kimaisha.
“Hawa wasichana walikimbia kukeketwa wamefanya maamuzi ya kweli na ni chachu ya mabadiliko, hebu tunzeni kumbukumbu zao kwa ajili ya kizazi kinachokuja” alisema mkurugenzi huyo wa kipinga vitendo vya ukatili wa kijinsia Duniani.

Akizungumzia tukio hilo Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari WanawakeTamwa Valeria Msoka alisema kuwa Taasisi za serikali ziwe mstari wa mbela katika kutetea wahanga wa matukio ya kijinsia.
Msoke aliongeza kuwa Ofisi ya Mkuu wa wilaya pamoja na kamada wa polisi mkoa wa kipolsi Tarime/Rorya hawana budi kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia na kuwanusuru wale ambao wateseka kutokana na imani potofu iliyojengeka kwa jamii kuwa mwanamke ni Mtu wa kupigwa tu. 
                                                               ….MWISHO..
Powered by Blogger.