WAANDAMANA IDARA YA MAJI KUDAI MALIPO WATAKA MUHASIBU AFUKUZWE KAZI.
WAANDAMANA IDARA YA MAJI KUDAI MALIPO WATAKA MUHASIBU
AFUKUZWE KAZI.
WAFANYAKAZI 8 wa Idara ya Maji na Usafi wa Mazingira
Wilayani Tarime mkoani Mara ambao ni vibarua wameandamana hadi ofisi za Maji
kudai mishahara yao ya mwezi uliopita jambo ambalo wamesema limesababisha
watoto wao wasiende shule kwa kukosa ada.
Wakizungumza
na gazeti ili nje ya Ofisi za idara ya Maji walisema kuwa Uongozi wa uliopo sasa wa Idara chini ya Muhasibu wake Haruni Kituri Amekuwa na mazoea ya kuwacheleweshewa malipo
huku akidaiwa kuwapunja mishahara yao tofauti na uongozi uliopita wa Marehemu
aliyekuwa Meneja wa Maji Sebastian Swima.
“Tunatakiwa
kulipwa mishahara au malipo yetu kila ifikapo 28 lakini mwezi unapitiliza hadi
sasa hatujalipwa fedha,Uongozi wa Marehemu Meneja Swima tulilipwa kwa wakati na
mshahara ulikuwa laki 273,000 lakini
sasa wamepunguza hadi laki 250,000”Alisema Kichere Chomete (40) Dereva wa Gari
la Idara ya Maji.
Joseph Iroma
(43) Mkazi wa Mtaa wa Kenyamanyori amabye ni milinzi wa
mashine ya maji Lambo la maji la Kenyamanyori kwa miaka 4 alisema kuwa
wanazungushwa malipo kwakuwa hawana mikataba ya kazi na amekuwa akilinda
mashine bila kuwepo kwa umeme na kumpa wakati mgumu kazini.
“Ungozi
Uliopo unasema sisi hatujasoma! Nawakati watu wamefanya kazi zaidi ya miaka 10
na bado ni vibarua kwahiyo wanataka watu wenye digree ndio waje wachimbe mitaro
ya kuweka mabomba! Huu ni unyanyasaji tumeshindwa hadi kupeleka watoto shule”
anasema Iroma.
Kaimu Meneja
wa Idara yamaji safi n usafi wa mazingira ambaye pia ni Muhandisi wa Maji
Halmashuri ya mji Tarime Dickson Kamazina alikiri kuwa ni kweli Vibarua wamekuwa
wakicheleweshewa malipo Tangu mwezi Novemba,2014.
Kamazina
Alisema kuwa sababu ya kucheleweshwa kwa malipo inatokana na makusanyo madogo ya maji na kuna wateja wa
maji 1,500 ambao hata hivyo wengi wao wana madeni ya maji na hawalipi fedha nakwamba
hakuna ruzuku kwenye idara hiyo.
“Mimi ni
Mgeni nimeingia Novemba nikakuta vibarua walikuwa hawajalipwa fedha za Novemba
nikashughulika ndani ya mwezi mmoja kulipa malipo ya miezi miwili, na makusanyo
ni madogo tunakusanya milioni 6 na tunawatumishi 18 malipo ni zaidi ya milioni
5 “alisema Kamazina.
Anaongeza”Fedha
hizo hizo bado tulipe ada, na matumizi ya umeme na mengineyo Hatuna ruzuku
unakuta fedha haitoshi inabidi ukusanye ikikamilika ndiyo ulipe vibarua ila leo
hii watawekewa fedha zao kwenye akaunti.
Akizungumiza
Mikataba Kamazina alisema kuwa amekuta vibarua hawana mikataba na sasa ana
anadaa mikataba ya vibarua nakwamba
vibarua si waajiriwa na malipo yao ni sh.8,000 kwa siku ambayo kuzikusanya na kulipwa baada ya mwezi, na kila
mtu analipwa kulingana na siku alizofanya kazi
nakwamba malipo yanatofautiana kulingana na miezi na siku walizofanya
kazi.
Hata hivyo Mgumo
Adrea alisema kuwa anasikitika licha ya kufanya kazi kwenye idara hiyo ambayo
ni ya Serikali bado analipwa kama kibarua, nakwamba malipo ya 8,000
yalishapanda ambapo kwa uongozi uliopita kila mtu alilipwa sh. Laki 273 elfu kwa kila mwezi.