Wawili wafariki dunia katika ajali za Barabarani



Wawili wafariki dunia katika ajali za Barabarani

WATU wawili akiwemo Mwanafunzi wa Darasa la tano Shule ya msingi Rwang’enyi Wilayani Rorya Mkoani Mara wamefariki Dunia kwa nyakati tofauti wakihusishwa Ajali za Barabara.

Akizungumzia matukio hayo Kamanda mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya ACP Lazaro Mambosasa alisema kuwa tukio la kwanza Mwanafunzi wa Darasa la tano shule ya msingi Rwang’enyi Benjamin Ismail 13 amefariki dunia Desemba10,2014 akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya KMT iliyopo Shirati baada ya kugongwa na mwendasha pikipiki ambaye hakujulikana na kjumsababishia majeraha sehemu za kichwani.

Kamanda huyo aliongeza kuwa Marehemu alikugongwa wakati akiwa anaenda shuleni kusoma wakati akiwa amepanda baisikeli anaendesha majira ya saa mbili asubihi.

Aidha Mambosasa aliongeza kuwa marehemu aligongwa na mwendesha pikipiki ambaye jina lake halikujikana na pia namba za usajili wa pikipiki hazikujulikana kwa urahisi kwa kuwa baada kuwa amegonga alikimbia na jeshi la pilisi linafanya jitihada za kumsaka na kumkamata ili kumfikisha kunako husika. 

Tukio jingine Mambosasa alisema kuwa pikipiki yenye namba za usajili MC 459 KBT aina ya SUNLG iliyokuwa ikiendeshwa na Daud Kinyunyi 20 mkazi wa kijiji cha Kabwana alimgonga mtembea kwa miguu Juma Peter 5 mkazi wa Raranya na kumsababishia kifo pao hapo.

Katika tukio hilo kamanda amesema kuwa Mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani ili kukabiliana na sheria punde upelelezi utakapo kamilika.

‘’Natoa wito kwa madereva wanaoendesha vyombo vya moto kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepusha vifo vya mara kwa mara na majereha na hata uharibifu wa vyombo vyao’’alisema Mambosasa.
Powered by Blogger.