Graca Michael Wazazi ondokeni na ukeketaji Tarime

Picha ya aliyekuwa mke wa Rais wa kwanza wa Afirika kusini Nelson Mandela akiongea na Wwanafunzi wa shule ya Msingi Masanga ni pamoja na Mabinti wa kike waliokimbia kukeketwa na kuifadhiwa katika kituo cha TFGM Masanga wilayani Tarime Mkoani Mara katika mwaka huu walikimbia mabinti 634.



Graca Michael Wazazi ondokeni na ukeketaji Tarime
Aliyekuwa mke wa rais wa kwanza Aafika kusini Nelson Mandela Mama Graca Machel ameitaka jamii kuondokana na suuala zima la ukatili wa kijinsia ukiwemo Ukeketaji, Ndoa za utotoni, ,Mimba za utotoni kwa lengo la kumulinda motto wa kike ikiwa ni pamoja na kutimiza ndoto zake.

Kauli hiyo imetolewa jana katika uwanja wa shule ya Msingi masanga kipindi akiongea na wananchi wanafunzi pamoja na mabinti ambao walikimbia ukeketaji katika musimu wa Tohara na kuweza kuifadhiwa katika kituo Termination Of Female Genital Multilation( TFGM) Masanga  wilayani Tarime Mkoani Mara.

Aidha Michel alisema kuwa kufanyika kwa vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto wa kike ni kumaliza ndoto zake.

“Hawa wasichana walikimbia kukeketwa wamaefanya maamuzi ya kweli na ni chachu ya mabadiliko hebu tunzeni kumbukumbu zao kwa ajili ya kizazi kinachokuja” aliseama.

Kwa upande wake mwakilishi wa shirika la  Mfuko wa idadi ya watu la umoja wa Mataifa (UNFPA) Dr Natalia Kanem amewataka watoto wasikate tama waweze kushikilia ndoto zao ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wazazi katika kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Ameongeza kuwa mwaka 2014 ulikuwa ni mwaka wa matumaini baada ya wazee wa kimlia kusema wameondokana na vitendo vya ukeketaji ikiwa ni pamoja wavulana kufanyiwa tohara bandala.

Pia ameongeza kuwa vyombo vya mahakama pamoja na polisi vitaendelea kupewa mafunzo juu ya kupinga vitendo vya ukatili kwa lengo la kukomesha kabisa.

“Tanzania ni Nchi ndogo lakinimaendeleo badao na  idadi ya watoto waliochini ya miaka 17 ni nusu ya watanzania kwahiyo hatuna budi kuwalinda watoto hao ikiwa ni pamoja na kuwalinda, kuwapenda na kuwathamini”aliseama.

Naye Mkuu wa wilaya ya Butiama Aangelina Mabura kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mara alisema kuwa kikubwa ni kuahakikisha watanzania wanaungana kwa ajili ya kukomesha ukatili kwa watoto wadogo na kuangalia kuwa kwanini wengine wanatoka mbali wanakuja kusaidia na jamii inaweza kukemea suala hilo na ikasikika.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tarime John Henjewele aliongeza kuwa Mama Grace Machel ameamua kufika Tarime baada ya kusikia kilio cha mtoto wa kike  ususani Tarime kwa lengo la kumkomboa Mtoto wa kikea ambayeamekuwa akinyimwa fursa muhimu ikiwemo elimu.

“Watoto wakike wa kitanzania wanakeketwa na kuwekewa kirema cha maisha kutokana na mila potofu zilizopitwa na wakati” alisena Henjewele.
                                           …Mwisho…
Powered by Blogger.