Waandishi wa habari Mushirikishe Mwenyezi Mungu.

Ni picha ya Mwandishi wa habari Sam Maela akiimba wimbo wa kusifu katika kanisa la EAGT Buhemba Wwilayani Tarime  Mkoani Mara.


 
Waandishi wa habari Mushirikishe Mwenyezi Mungu.
Waandishi wa habari wametakiwa kumshirikisha mwenyezi mungu katika maisha yao kwa lengo la kufanikiwa zaidi suala ambalo litapelekea wandishi kuandika habari za kweli zisizokuwa na uchonganishi ndani yake ambayo yanaweza kusababisha machafuko ya nchi na watanzania wakaanza kumwaga damu pasipokuwa na sababu za msingi.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mmoja wa waandishi wa habari ambaye pia ni Mwimbaji wa Nyimbo za injiri na ni mhubiri Bw: Sam Maela kipindi akitoa maubiri katika kanisa la EAGT Buhemba wilayani Tarime Mkoani Mara.

Samu Maela alisema kuwa waandishi wa habari wamekuwa wakitumiwa vibaya na baadhi ya viongozi wenye kutaka maslahi yao binafsi kwa sababu yakutomushirikisha mwenyezi mungu katika kazi zao.

“Tangu nimeokoka na kuanza kumushirikisha mwenyezi mungu nimeweza kubadili maisha yangu kwa kiasi kikubwa”alisema Maela.

Aidha Maela alitumia Nafasi hiyo  kuwaombea wagonjwa mbalimbali kwa ajili ya kuwaombea huku akiwataka kuwa wasikate tama kwani mwenyezi mungu yupo kwa ajili ya kusaidia watu wenye mahitaji maalumu.

Kwa upande wake Mchungaji wa kanisa la EAGT Buhemba Thomas Rioba aliwataka wazazi kulea watoto wao katika misingi ya kidini huku akiwataka vijana kumushirikisha mwenyezi mungu katika kazi zao kwa lengo la kupata maisha bora yenye kumutukuza mwenyezi mungu.

“Mfano ni kama vijana wa leo ambao wameweza kumuheshimu mwenyezi mungu na kukabidhi maisha yao kwa mwenyezi mungu kwa kuweza kutangaza uchumba wao rasmi kanisani” alisema Mchungaji Rioba.

Mchungaji alisema kuwajamii ikimushirikisha Mwenyezi mungu katika maisha yao itasaidia sana nipamoja na kubadili maisha yao waliyonayo kwani wengi wameweza kukata tama sula ambalo halimupendezeshi mwenyezi  Mungu.
                                             ……Mwisho…


Powered by Blogger.