wauana wakigombania Ardhi. Ndugu




MKAZI  wa kitongoji cha Nyamirungu Kijiji cha Magoma kata ya Binagi Wilayani Tarime Mkoani Mara ameuawa kwa kukatwa mapanga na ndgu wa Damu wakigombania Mipaka ya Ardhi

Akisimlia tukio hilo kwa waandishi wa habari Ofisini kwake Kamishina msaidizi wa Jeshi la polisi wa Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya Lazaro Mambosasa alisema kuwa tukio hilo lilitokea November,14 mwaka huu majira ya saa 2.00 asubuhi.

Aidha Mambosasa alimtaja marehemu kuwa ni Samweli Mgaya Waitte 44 ambaye aliuawa na Mkubwa wake Chacha Mwita Waitte 56 wakati wakigombania mipaka ya Ardhi na kuwa wote ni wakazi wa Kijiji cha Magoma.

Mambosasa aliongeza kusema kuwa baada ya ugomvi huo kutokea Mtuhumiwa alimshambulia kwa mapanga marehemu ambapo alishambuliwa kwa kukatwa sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani na tumboni na kusababisha kifo chake papo hapo.

;;Marehemu  alimkata mapanga mtuhumiwa na  kumjeruhi sehemiu mbalimbali za mwili wake hali ambayo ilisababisha kwenda kulazwa katika hospitali ya halmashauri ya Mji wa Tarime akiwa chini ya uangalizi wa polisi ili akipona akahojiwe;;alisema Mambosasa.

Kamanda huyo ameitaka jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi badala yake wapeleke matatizo katika vyombo vya sheria hususani katika mabaraza yanayo husika na Ardhi ya vijiji ili kuweza kutatua migogoro inayowakumba.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
  
Powered by Blogger.