Akina Mamajitokezeni kugombea Uongozi.
Akina mama
wametakiwa Kujitokeza katika kugombea uongozi kupitia nyadhifa mbalimbali ili kuweza kutetea haki
zao za ,msingi ikiwa ni pamoja na kutimiza haki ndoto zao za uongozi.
Kauli hiyo
imetolewa na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Tarime na Halmashauri ya willaya ya
Tarime ambaye kwa sasa ni Diwani wa kata
ya Itiryo Charles Mwera Nyanguru kipindi akiongea na gazeti hili.
Charles
alisema kuwa akina mama hawana budi kuchukua fomu za kugombea katika chaguzi za
serikali za mitaa kwani wanawake wamekuwa wakipoteza fursa ambazo ziko wazi kwa
kuogopa kugoimbea.
“Wakina mama
wakigombea watatumia fursa hizo kuzidi kutetea haki zao za msingi na si
kutegemea wanaume kwa kila kitu” alisema Nyanguru.
Hata hivyo
Mwera aliwataka vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftri la
kudunmu la wapiga kura.
“Kujiandikisha
katika daftari ndo nguzo kubwa ya kukufanya upige kura na kupata kiongozi bora
hivo basi vijana wajitokeze katika kujiandikisha kuanzia 23 novemba mpaka 29
novemba mwaka huu alisema” Mwera.
Aaidha
aliongeza kuwa vijana ndio tegemeo la taifa hivyo waondokane na ushabiki wa
vyama na kufanya maamuzi yaliyoya kweli katika kuchagua viongizi waliobora ili
kuletea Taifa maendeleo.
“Naweza kutoa
msisitizo kuwa na vijana waweze kujitokeza kuchukua fomu za kugombea si
kuwaachia wazee tu” alisema .
….MWISHO…