Ligi ya Mbunge wa viti maalumu kutimua vumbi Novemba 23.
Ligi ya Mbunge wa viti maalumu
kutimua vumbi Novemba 23.
Kupitia rigi
ya Ester Matiko Tarime Football
Rising Stars Cup 2014- 2015ambaye ni
mbunge wa viti maalumu tiketi ya chama
cha Demokrasisia na maendeleo Chadema itaanza kutimua vumbi kuanzia 23 novemba katika viwanja tofauti kwa kukutanisha timu
mbalimbali za kata 32 zilizomo ndani ya Mji wa Tarime na wilaya Tarime Mkoani Mara kwa lenngo la kusaka
vipaji kutoka maeneo ya Vijijini.
Awali ya
hapo mdhamini wa mashindano hayo ambaye ni mbunge vwa viti maalumu Jimbo la
Tarime Ester Matiko ameweza kutoa mpira
mmommoja kwa kila timu kupitia timu32 kwa ajili ya mazoezi kabla ya kuanza
kwa michuano hiyo.Ester Matiko amesema
kuwa ameamau kuanziusha ligi hiyo ili kuweza kukutanisha vijana huku wakiibua
vipaji vilivyojificha na kutengeneza timu moja atakayoiendeleza mpaka
inashiriki michuano ngazi ya mkoa.
“Lengo langu
ni kuibua vipaji na kuweza kupata timu moja ili niweze kuiendeleza ili iweze
kucheza katika ngfazi ya mkoa” alisema Matiko.
Martini Kebacho ni Mratibu wa michuano hiyo wakati
akikzungumzia michuano hiyo alisema kuwa ratiba tayari imetolewa kwa timu
zote32 ambazo zitashiriki awamu ya kwanza ili kupata timu16 na kucheza hawamu
ya tatu ili kupata timyu8 ambazo zitaanza ligi ili kupata mshindi wa kwanza
mpaka wa tatu.
Mdhamini swa
mashindano hayo alisema kuwa mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha
shilingi million moja na kombe Mshindi
wa pili Laki saba na mipira miwili, huku Mshindi wa tatu akijinyakulia na mpira
mmoja na zawadi mbalimbali kwa wachezaji bora, wafungaji bora na walinda
miilango bora.
Hata hivyo
matiko amewataka wananchi kutoingiza siasa kwa kutumia itikadi za vyama bali
washiriki mashi ndano hayo ni kwa watu wote ili kuweza kusaka vipaji kupitia timu za vijijini.
….Mwisho…