Kiribo limited watoa msaada wa Mllioni 2.5.
Kiribo limited watoa msaada wa
Mllioni
Katika kuunga
juhudi za serikali ili kuboresha sekta ya Elimu kupitia shule za msingi kampuni
ya kiribo Limitedi kupitia mkurugenzi wake Kebacho Monata imetoa imetoa vifaa mbalimbali
katiki shule ya Msingi Nyakunguru “B”Wilayani Tarime Mkoaniu Mara yakiwemo
Madaftari 1000 Tanki la Maji lenye Ujazo wa Lita 2000 Kalamu Box 2 ikiwemo na
Vifaa vya Michezo vyenye jumla ya Shilingi Millioni2.5.
Katika
kukabidhi vifaa hivyo mbele ya Mgeni rasmi Meneja mgodi wa North Mara Garry
CheapMan ,Samwel gasaya kwa niaba ya mkurugenzi wa Kilibo limited Bw Kebacho
Monotha anasema kuwa kutolewa kwa msaada huo ni moja ya kuunga juhudi za
serikali katika kuboresha sekta ya elimu ususani katika shule za Msingi.
“Tumeamua
kurudisha asilimia ndogo ya faida
tunayoipata kutokana na uwekezaji ndani ya Mgodi wa North Mara”alisema
Gasaya.
Gasaya aliongeza
kuwa mkurugenzi wa kampuni ya Kiribo ameamua kurudisha faida anayoipata kwa
wananchi ili kuzidi kuleta mahusiano mema kama mwekezaji mzawa na kuweza kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabiri
wanafunzi wa shule za msingi zinazozunguka mgodi wa dhahabu wa Nyamongo.
Meneja wa
Mgodi wa Dhahabu wa Nyamongo African Barrick Gold Mine (ABG) North Mara ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika kukabidhi masaada huo anasema kuwa huo ni mfano
mzuri na kuomba kuzidi kuendeleza kazi za pamoja huku akiwatakma
wakandalasi kutimiza ahadi zinazotolewa kwa wananchi ili
kuendeleaza mahusiano mazuri.
“Huu ni
mfano mzuri unaoonesha wawekezaji wazawa jinsi wanavyosaidia katika sekta ya
elimu” alisema Garry chapman.
Kwa upande
wake Mwalimu mkuu wa shule ya Nyankunguru B Mwl Donitha Mwita alitoa shukrani kwa kampuni
ya Kiribo limited pamoja na mgodi wa North Mara kwa kuzidi kuunga juhudi za serikali katika
kuboresha sekta ya Elimu.
Aaidha
mwalimu huyo aliomba mgodi huo kuendelea kutoa msaada ikiwa ni pamoja na ujenzi
wa nyumba za walimu pamoja na ukarabati wa madarasa kwani madarasa hayo
yamechakaa sana.
“Shule yetu
imetelekezwa kwa mda mrefu jaribuni kutusaidia katika kukarabati madarasa ili
kuboresha madarasa”alisema Mwalimu mkuu.
Shule ya
Msingi Nyakunguru B ina jumla ya wanafuzi 520 wasichana kwa wavulana nyumba za
walimu4 kati ya 12 madarasa 9 kati ya 12 ambapo changamoto kubwa katika shule
hiyo ni uchakavu wa majengo na upungufu
wa nyumba za walimu.
…….Mwisho….