Kipato duni chanzo cha utoro shule za Sekondari
Kipato duni chanzo cha utoro shule za
Sekondari
Imebainika
kuwa kipato duni kwa baadhi ya wazazi na walezi wilayani Rorya mkoani Mara ni
chanzo kikubwa cha utoro katika shule za
sekondari, ikiwa ni pamoja na mwamko mdogo wa Elimu kwa wazi.
Kauli hiyo
imetolewa na Mwl mkuu Joshua John
Mzori katika shule ya sekondari Buturi Wilayani
Rorya Mkoani Mara kwenye mahafari ya 16 kidato cha Nne iliyofanyika hivi
karibuni shuleni hapo.
Mwalimu mkuu
alisema kuwa baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakiacha shule na kujiingiza katika
sula zima la ujasiliamali ili kuweza kupata kipato cha kutunza familia.
“Baadhi ya
Wazazi na walezi kipato chao ni kidogo hivyo utumia fursa hiyo kuwaruhusu
wanafunzi kujiingiza katika sula la ujasiliamali na kuondokana na Masomo”
alisema Mwalimu mkuu.
Zedekia Oloo
Siso kwa niaba ya mgeni rasmi mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Ya
Rorya Samwel Kiboye Maarufu kama Namba Tatu aliweza kuendesha harambee katika maafari hayo ili kuweza kuongeza nguvu
katika ujenzi unaoendelea wa mahabara ambapo wazazi hawakuonesha moyo mkubwa wa
kuchangia ili kuweza kuandalia wanafunzi mahalli pazuri pa kusomea.
“Kulingana na juhudi nilizozifanya kwa kuchangisha
katika maafari haya bado wazazi wameniangusha” alisema Zedekia.
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Bodi wa shule ya Sekondari Buturi iliyopo Wilayani Rorya Mkoani
Mara John Olala Kolimba alisema kuwa
amekuwa mwenyekiti atangu kufunguliwa kwa shule hiyo mpaka sasa ni mwaka wa 8
amedai kuwa waliamua kujenga hosteli shuleni hapo ili kuondoa changamoto zinazo
wakumba watoto wa kike na kupelekea kukatisha masomo.
Shule ya
sekondari Bjuturi iliyopo Rorya mkoani Mara ina jumla ya wanafunzi 365 kwa
upoande wa wahitimu walioitmu shuleni hapo ni 44 huku wasichana wakiwa 18n
na wavulana 26 na ambao walijiandikisha
kufanya mtihani ni wanafunzi 48 na waliobahatika kufanya Mtihani na 44 pia
shule hiyo inakumbwa na changfamoto ya ukosefu wa maji pamoja na walimu wa
masomo ya sayansi.
…………………………………Mwisho……