Auawa kwa kuchomwa kisu kifuani


MKAZI wa Mjini Tarime Mkoani Mara Mwita Matutu 28 ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani upande wa kulia na kufa papohapo na Chacha Marwa Mapengo 30 wa Sirari.

Akizungumzia tukio hilo kwa waandishi wa habari kamishina msaidizi wa jeshi la mpolisi mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya ACP Lazaro Mambosasakwa alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira saa 3.45 usiku wa kuamkia Novembea 19,mwaka huu.

Aidha Mambosasa aliongeza kuwa chanzo cha kuchomwa kisu marehemu ni ugomvi uliozuka baina ya marehemu na Chacha MWITA Mapengo Wa sirari wakati wakiwa wanakunywa pombe katika Bar ya Chirs Pamp ya mijini hapa.

‘’Natoa wito kwa wananchi kuacha mara moja kujihusisha na vitendo vya vurugu kama kuna tofauti wazifikishe sehemu husika ili ziweze kushugulikiwa’’alisema Mambosasa.

Kamanda huyo aliongeza kuwa jeshi la polisi lina mshikilia na kumhoji mtuhumiwa punde upelelezi utakapo kamilika atafikishwa mahakamani ili kukabiliana na shitaka.
………………………………………………………..mwisho………………………………

Powered by Blogger.