Auawa kwa mapangaTarime



 Auawa kwa mapanga Tarime
Mtu  mmoja aliyejulikana kwa jina la Matiku Makenge Ghati  mwenye umri wa miaka 50 mkurya mkulima mkazi wa kitongoji cha Ngalamu kijiji Rosana kata ya Nyarerero wilayani Tarime Mkoani Mara ameuawa kwa kutatwa mapanga sehemu za kichwani mapanga nawatu wasiojulikana na kusanbabishiwa kupoteza maisha yake.

Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime Rorya  Kamishena msaidizi wa jeshi la polisi Benedict Lazaro Mambosasa amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema kuwa marehemu alivamiwa Novemba 19 karibu na nyumba yake kipindi akitoka matembezini na kushambuliwa kwa mapanga.

“Kutokana ka tukio hilo  hatujabaini mtuhumiwa yeyote lakini badoijeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini wahuska na kuchulua hatua dhidi yao” alisema kamanda.

Mambo sasa aliongeza kuwa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika hospitali ya mji wa Tarime kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Aaidha kamanda huyo ametoa wito kwa jamii kuwa wajijengee tabia za kutoa taarifa pale wanapoona vitendo vya kiarifu vinatendeka ili jeshi la polisi liweze kufika mara moja na kuwatia mikonono waharifu hao.

Sanjari na hayo lazaro almesisitiza suala la Amani ususani tunakoelekea katika chaguzi za serilai za mitaa.

“Tunaelekea katika chaguzi wananchi tutunze amani na viongozi wasiingilie wananchi ili kuwarubuni bali waache wakachague viongozi wanawapenda” alisema kamanda.
                                            …Mwishoi…
Powered by Blogger.