Makambazi wawili raia wa Kenya wauawa na wananchi Tarime
Makambazi wawili raia wa Kenya wauawa na
wananchi Tarime
Watu wawili wanaoaminika kuwa raia wa Kenya
wameuwa na wananchi Wilayani Tarime kwa kushukiwa kuwa ni majambazi baada
ya kuhisiwa kuiba pikipiki na kuificha ndani ya nyumba anayoishi mmoja wa
majambazi hao.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 12
asubuhi katika kitongoji cha Sokoni kijiji cha Sirari kata ya Sirari Wilayani
hapa kwa wananchi kufanya dori katika mji wa Kebwe Lokobo 42 mwanamke aliyekuwa
akiishi na mmoja wa majambazi hao kama mpenzi wake.
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime Rorya
kamishina msaidiozi wa polisi Lazaro Mambosasa alithibitisha kutokea kwa kutio
hilo na huku waliwaawa wakitajwa kuwa ni Joel Mwita (27) mkazi wa Maabela na
Samwel Mwita (25) mkazi wa Maeta wote nchini Kenya.
Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika
chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime ikisubiri
familia kwa utambuzi na kwa maziko.
Mwenyekiti wa kijiji cha Sirari Nyangoko Romani
alisema kuwa Oktoba 11 alipata taarifa kutoka kwa mwanakijiji wake Chacha Monanka
kuwa usiku wa kuamkia siku hiyo alivamiwa na majambazi nyumbani kwake na
kunyanganywa pikipiki aina ya SunLG lakini wakahisi vijana hao wawili kuhusika.
“Tuliitana kufanya doria kuanzia saa moja na
nusu usiku tukazingira nyumba aliyokuwa Samwel Mwita ilipofika saa 11 alfajiri
tulimgongea na kumtoa nje baada ya kuhojiwa alikiri na kutupeleka
kwa mwenzake Joel Mwita ambapo walisema walipoificha pikipiki ile” alisema
Roman na kuongeza:
“Niliwaomba wananchi wasiwashambulie kwanza ili
tupate kuwahoji na kupata mtandao wote, lakini hali ilibadilika hata mimi na
wenzangu tukapigwa mawe na kuamua kukimbia wananchi wakavunja mlango na kuitoa
pikipiki nje na kwa kutumia magodoro na vyandarua wakawaasha moto” alisema.
Kufuatia hatua hiyo Kebwe Lokobo (42) alitoroka
na kuingia kwenye gari la polisi kujisalimisha baada ya mpenzi wake kufahamika
kuwa ni mwizi huku yeye akimhifadhi na vitendo vuya ujambazi kuongezeka katika
eneo hilo la Sirari.
“Zaidi ya pikipiki 13 zimeporwa lakini
alipohojiwa wamesema wamehusika kwenye matukio manane kwa kuiba pikipiki aina
ya SunLG 3, Boxer 3 na pvs 2 zote wanaenda kuziuza rift valley nchini Kenya”
alisema Mwita Rhobi.
Mwisho.