Kabaka azindua kampeni za kupinga ukeketaji Tarime.
Picha ya Mama kabaka baada ya kukata utepe katika uzinduzi wa kampeni za kupinga Ukeketaji na Ndoa za Utotoni Tarime
Waziri wa
kazi na ajiri Gaudensia Kabaka amezindua kampeni za kupinga Ukeketaji pamoja na
ndoa za utotoni katika wilaya ya Tarime mkoani Mara.
Uzinduzi huo
ambao umeambatana na sherehe za mtoto wa kike duniani ambazo uazimishwa kila
mwaka Okitoba 11kwa lengo la kutetea haki ya mtoto wa kike kwani amekuwa
akinyimwa haki zake za msingi kulingana na vitendo vya unyanyasaji
anavyofanyiwa huku kauli mbiu ikisema kuwa kumwawezeshawasichana kumaliza
kumaliza mduara wa ukatili.
Kampeni hizo
kitaifa zilizinduliwa jijini Dar es salaam mnamo Agosti mwaka huu na waziri wa
Maendeleo ya jamiij jinsia na watoto, Mama Graca Machel mtetezi wan a mwanaharakati wa kutetea
haki za watoto wa kike duniani.
Shere hizo
ambazo zimefanyika katika viwanja vya tarafa ya Inchugu kata ya Sirari wilayani
Tarime kabaka alisema kuwa jamii haina budi kukubali mabadiliko kwa lengo la
kukomboa mtoto wa kike.
Gaudensia aliongeza kuwa kumkeketa mtoto wa kike ni moja ya
chanzo cha kumuandaa katika ndoa za
utotoni kwa hali hiyo jamii inatakiwa kuondokana na mila hiyo potufu ili kumpa
mtoto wa kike nafasi ya kuendelea na masomo.
’Wakati wa
mababu zetu wanadhimisha saro walikuwa na maana nzuri lakini katika kipindi
hiki cha kizazi kipya mila hiyo imepitwa
na wakati kwa kuzingatia kuwa kuna mchanganyiko wa makabila na nikizazi cha
Dotikomu’’alisema kabaka.
Kwa upande
wake mwakilishi wa Waziri wa jinsia na
watoto Sophia Simba Bernard Mwisanya alisema kuwa haki sawa ya mwanamke
inayodaiwa haitapatikana kama jamii haiko tayari kuondokana na Vitendo vya
ukatili dhidi ya mtoto wa kike.
Aidha Mkuu
wa wilaya ya Tarime John Henjewele alizidi kuonya jamii kuondokana na kutumia
nyara za serikali bila kibali na kuwa hatua kali zitachukuliwa
dhidi ya wale watakaozitumia bila kibali cha serikali.
Naye mkuu wa
wilaya ya Butihama Angelina Mabura alitoa rai kwa wazazi wenye tama na mali kwa
kuozesha mtoto wa kike ili waweze kubadili maisha yao kuondokana na vitendo hivyo mara moja.
“Watoto
endeleeni kupaza sauti ukisikia baba,
Babu, Shangazi anapanga kukukeketa paza sauti tutasikia mara moja na kufanyia
kazi kilio chako” alisema Mabura.
Sanjari na
hayo Mkurugenzi wa jukwaa la utu wa
mtoto (CDF) Mtandao Koshuma Mtengeti alisema lengo la kufunguliwa kwa kampeni
hizo ni kuendelea kuwekezesha wasichana kwa kuwajengea uwezo wawao ili kuweza
kusimamia haki zao na kupaza sauti zao juu kwa mambo ambayo yanawahusu na
kuweza kutoa taarifa pale haki zao zinapovunjwa .
Kauli mbiu
yetu leo inasema kuwa “kupinga ukeketajina ndoa za jutotoni ni jukumu letu sote”
hivyo kila mtu anayonafasi ya kumlinda mtoto wa kike ili aweze kutimiza ndoto
zake.
Aidha
Mtengeti alizidi kusemakuwa Jukwa la utu wa mtoto (CDF) Mtandao wataendelea na
zoezi la kukuza uelewa wa wananchi juu ya madhara ya ndoa za utotoni na
ukeketaji hususani wazazi na jamii kwa ujumla ili kutokomeza vitendo hivyo.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya kamishena msaidizi Lazaro Mambosasa alizidi
kuhasa jamii kwa ujumla kuendeleza ujasiri wa kutoa taarifa na kuongeza kuwa
madawati ya jinsia yatazidi kufanya kazi kwa ufasha ili kutimiza ndoto za mtoto
wa kike huku akitoa onyo kwa Ngariba watakao fanya vitendo vya ukeketaji.
“Hapa nilipo
tayari nina majina ya Ngariba na baadhi wamejisalimisha kwangu tutawakamata na
kuwachukulia hatua” alisema Kamanda.
Wakati huo
huo mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA) Valerie Msoka
alizidi kupongeza vyombo vya habari kwa mchango mkubwa walionayo katika kuibua
na kuandika changamoto zinazowakumba watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia.
“Vyombo vya
habari ni chachu kubwa tuzidi kuvitumia ili kuibua zaidi
changamotozilizojificna” alisema Msoka.
Kampeni hiyo
iliyozinduliwa ili kupinga ukeketaji imelenga jamii ya Tarime kuondokana na
vitendo hivyo kwani mwaka huu ni mwaka wa kukeketa na imesimamiwa na Shirika la jukwaa la utu wa
mtoto kwa ki ushirikiana na
mashirika mbalimbali kam vile Chama cha waandishi wa habari TAMWA, UNFPA, Child
Marriege Free Zone huku jeshi la Polisi
Halmashauri za wilaya na Mji zikionesha ushiriki mkubwa kwa lengo la
kufanikisha Zoezi hilo
…..Mwisho…