Nyamisangura Sekondari wamwagiwa vitabu vya sayansi na kampuni ya airtel
Kaka mkuu wa shule ya Nyamisangura iliyopo wilayani Tarime Mkoani Mara akikabidhiwa vitabu na Meneja wa kampuni ya aitel mkoa wa Mara Joseph Mushi kwa niaba ya wanafunzi kulia kwake ni Ofisa masoko kanda ya ziwa Emmanuel Raphael
Shule ya
sekondari Nyamisangura wilayani Tarime Mkoani Mara wamepata msaada wa vitabu
vya masomo ya Sayansi vyenye thamani ya
zaidi ya shilingi millioni nne kutoka katika kampuni ya mtandao wa simu
za aitel Tanzania kwa lengo la kuinua masomo ya sayansi katika shule za
sekondari.
Katika
kukabidhi msaada huo wa vitabu vya masomo ya sayansi Joseph Mushi ambaye ni
meneja wa kampuni hiyo mkoa wa Mara alisema kuwa kutolewa kwa msaada huo ni
kila mwaka.
“Kila mwaka
kampuni yetu hutoa msaada wa vitabu kipindi hiki tumejikita katika sekta ya
elimu ususani vitabu vya masomo ya sayansi kwa ajili ya kuinua masomo ya
sayansi katika shule za sekondari” alisema Meneja.
Meneja mkoa
aliongeza kuwa kutolewa kwa msada huo ni kwa sababu ya mchango mkubwa wa jamii
katika kuchangia kampuni hiyo kupitia ununuzi wa maongezi hivyo asilimia Fulani
urejeshwa kwa jamii ili kuweza kusapoti huduma za kijamii.
Naye Meneja
masoko kanda ya Ziwa Emmanuel Raphael aliwataka wanafunzi hao kutunza vitabu
hivyoi ikiwa ni pamoja na kuzidi kupenda masomo ya sayansi.
“Tunategemea
wanganga kupitia Nyamisangura hivyo endeleni na moyo wa kupenda masomo ya
Sayansi” alisema Meneja kanda.
Kwa upande
wake mkuu wa shule ya Sekondari Nyamisangura Jolijo Zephania alitoa shukrani
kwa niaba ya wazazi na kuzidi kuomba kampuni nyingine kujitkeza ili kuweza
kutoa msaada.
“Shule bado
ina mahitaji mengi kulingana na changamoto tulizozisoma mbele ya Mgeni rasmi”
alisema Mkuu wa shule.
Ofisa elimu
msaidizi katika Halmashauri ya Mji wa Tarimea Wegoro Mtarasha ambaye pia
alikuwa mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Venance Mwamengo
alizidi kusisitiza walnafunzi hao kuazima vitabu kwa lengo la kuvisoma
Najua
wengine mutaazima vitabu hivi kwa ajili ya kutunza nyumbani kwenu azimeni kwa
ajili ya kusoma alisema Ofisa elimu msaidizi
Joseph Chacha ni kaka mkuu wa shule hiyo kwa
niaba ya wanafunzi alisema kuwa watatumia vitabu hivyo kwa lengo la kujiongezea
uelewa zaidi na kuzidi kuomba makampuni kuzidi kuwa na moyo wa kutoa misaada
ili kusaidia serikali.
……Mwisho….