Jamii saidieni wanaishi katika Mazingira hatarishi
Picha ya Mwanasheria wa kituo cha Center For Widows and Children Assistance (CWCA)Bw: Ostack Mligo kilichopo
Mjini Musoma Mkoani Mara kipindi akiongea na mmiliki wa blog ya Cleonews tz kuhusiana na changamoto zinazowakumba katika utendaji kazi.
Jamii imetakiwa kusaidia watu
wanaishi katika mazingira hatarishi kwa lengo la kuwaondolea msongo wa mawazo
kwani watu hao wakati mwingine uchukua maamuzi magumu baada ya ugumu wa maisha
na kutaka kujiondoa uhai wao.
Kauli hiyo ilitolewa na
mwanasheria mwandamizi wa kituo kisikuwa cha serikali Center For Widows and
Children Assistance (CWCA) kilichopo Mjini Musoma Mkoani kipindi akiongea na
gazeti hili ofisini kwake Mara Bw: Ostack Mligo.
Aidha Mligo amesema kuwa watu
wenye uwezo na kipato kikubwa cha fedha hawako tayari kusaidia jamii yenye
shida wakiwemo watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi suala ambalo
linazidi kuwa changamoto,
Ameongeza kuwa shirika hilo
linatoa msaada wa kisheria linasaidia watoto wanaoishi katika mazingira
hatarishi akina mama wajane ambapo kwa sasa mabinti 94 wamefanikiwa kupelekwa
vyuo vya ufundi kupitia shirika hilo.
Sanjari na hayo mwanasheria
amesema kuwa serikali haina budi kuwamstari wa mbele kwa kushirikiana na
Mashirika mbalimbali ili kuweza kupambana na vitendo vya ukatili vinavyoendelea
nchini hapa
Hata hivyo Mwanasheria
amezitaja changamoto wanazokumbana nazo kuwa ni hali ngumu ya maisha kwa watu
wanaitaji huduma ya kusaidiwa kwani uhitaji fedha ili kuweza kufuatilia kesi
zinazokuwa zinaendeshwa katika maeneo mbalimbali
……Mwisho…