Wanawake wadai haki sawa
Wanaharakati wakiwa katika kongamano la TGNP Mtandao wakiwana mabango yenye ujumbe jana ni katika ofisi za Tgnp Mtandao jijini Dar es salaam.
Wanawake wadai haki sawa
Wana harakati kutoka katika mikoa mbalimbali wakiungana na
mtandao wa jinsia Tgnp jijini Dar es salaamu
wamehungana kwa pamoja na kupaza sauti ya pamoja ili kudai haki sawa kupitia kongamano lililofanyika katika viwanja
vya Ofisi za TGNP Mtandao jijini hapa ikiwa ni nipamoja na kuzungumzia mambo ya
bunge maalumu la kubainisha
yatakayofanyika baada ya Bunge maaalumu
la katiba kumaliza Octopber 04 Mwaka
huu.
Kongamano hilo liliusisha baadhi ya waandishi wa habari
kutoka mikoa kama ukiwemo mkoa wa Shinyanga, Mara na Morogoro pamoja
nawanaharakatikutoka mikoa mbalimbali hapa nchini yakiwemo makundi maalumu ya
watu wenye ulemavu Makundi kutoka vituo vya juhudi na maarifa vinavyowakilisha Tgnp Mtandao
katika mikoa mbalimbali.
Lilian Liundi ni kaimu mkurugenzi wa Tgnp mtandao katika
kuwasilisha mada kwenye kongamano hilo alisema kuwa endapo Bunge maalumu la
katiba litapitisha rasimu ya katibainayopendekezwa kwa wingi wa kura za ndiyo za wajumbe wa Bunge
hilo, Mh Rais Jakaya Mrisho kikwete atakabidhiwa rasimu hiyo na kuwa katiba
inayopendekezwa
Aidha kaimu mkurugenzi alisema kuwa hatua itakayofuata kwa mujibu wa sheriaya
mabadiliko ya katiba ni utoaji wa elimu na uhamasishaji kwa umma juu ya maudhui
yaliyomo kwenye katiba inayopendekezwa kwenye katiba inayopendekezwa na kampeni
ya upigaji wa kura ya maoni.
“Sisi kama wanaharakati hatuna budi kuwa mabalozi wazuri ili
kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii ususani maeneo ya vijijinia”lisema
kaimu mkurugenzi.
Tgnp Mtandao wa wanawake na katiba pamoja na Mashirika yenye
kupigania haki za Watanzania wataendelea kutumia fursa zilizopo ili kufikisha
ujumbe uliokusudiwa ili kuelimisha jamii na kuelewa kuhusu katiba
inayoppendekezwa ili kusaidia wakati wa kupigia kura maoni juu yakatiba
hatimaye wapige kura wakiwa na maamuzi sahii.
Licha ya hayo wanaharakati hao wamezidi kusoisitiza suala
zima la 50 / 50 ili kuweza kuimarisha msingi wa wa usawa
“Tunatarajia katika
marekebisho ya katiba ya mwaka 1977 itakayotumika katika uchaguzi kwenye
marekebisho asilimia ya 50/50 iwepo “walisema.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
wanawake katiba Prof Ruth Meena alisema kuwa kama wanawake watazidi
kupambana ili yale waliyopendekeza katika rasimu ya katiba yaweze kuwekwa na
kubainisha
Alisema kuwa wanawake wamekuwa wakiwekwa pembeni pale
panapotokea ushindi hivyo mwanamke hana budi kushiriki katika mapambano yeyote
ili kuweza kupata haki zake za msingi
Wanawake tuweze kuunganisha nguvu ya pamoja na kuweza
kupambana na matendo ya unyanyasaji yanayojitokeza dhidi ya mama na motto.
“Pia wanawake katika
kongamano hilo wametakiwa kujitokeza kogombea nafasi za ngazi za juu kuanzia uraisi na si kupigania nafasi za chini” walisema.
………Mwisho….