Akina mama jitokezeni kwa wingi kujiandikisha katika dafrari la wapiga kura.
Picha aliyekuwa Mwnyekiti vijana Taifa John Heche kulia kwake ni Katibu wa vijana Bavicha Tai fa Mwita Jackson katika mkutano uliofanyika jana kwewnye viwanaja vya Serengeti wilayani Tarime Mkoani Mara
Akina mama
wilayani Tarime mkoani ,Mara wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha
katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuweza kufanya maamuzi ya kweli katika uchaguzi ujao.
Kauli hiyo
ilitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) wilaya Julius Ngoto katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika
viwanja wa Serengeti Mjini Tarime Mkoani Mara.
Alisema kuwa
akina mama ndo waliowengi wenye kufanya mapinduzi ya kweli hawana budi
kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha kwa wingi ili kipindi cha kupiga kura
waweze kufanya maamuzi.
Naye katibu
wa Baraza la Vijana Taifa ( BAVICHA) Mwita Jackson alilaani vitendo vinavyozidi
kufanywa na jeshi la polisi kwa kuonea wananchi na kusema kuwa jeshi la polisi
halina budi kutafuta namna ya kuishi na jamii ili kuondoa uasama.
“Kila siku
tunapiga kelele kuhusiana na mauaji ya jeshi la polisi na vijana wa Mgodini
lakini bado” alisema Katibu.
Kwa upande
wake aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana Taifa John Heche aliwasisitiza wananachi
kupitia rasmu ya katiba iliyopitishwa na kufanya maamuzi yao bila kushinikizwa
na kitu chochote.
“Katiba ndo
kila kitu nyie wananchi mtakapoletewa rasmu kutoa maoni fanyeni maamuzi yenye
kuleta mabadiliko ya Taifa ili kuweza kukomesha wale wenye nia mbaya na Nchi
yetu” alisema Heche.
Hata hivyo
katibu wa Chama hicho ngazi ya Wilaya Mwl Chacha Heche alisema kuwa jeshi la
polisi halina budi kujitazama kwa upya na kuondokana na manyanyaso kwa
wananchi.
“Tumepewa
ridhaa ya kuongoza na wananchi hivyo tutazidi kupambana mpaka haki yao
inapatikana” alisema Mwenyekiti John.
….Mwisho….