Sheikh Addulhakim Mrisho soud wanasiasa vusheni nchi kwa Amani.
Picha ya Sheikh wa wilaya Abdulhakim Mrisho Soud katika msikiti wa
ijumaa Bakwata akikabidhiwa msaada wa mabati kushoto kwake ni ktibu
msaidizi wa Chama Cha Mapinduzi wilaya Kapis Adogo akikabidhi msaada huo
wa mabati 45 yenye thamni ya shilingi laki tano na elfu tano kwa niaba
ya mbunge wa jimbo laTarime Nyambari Nyangwine wengine ni vingozi wa
(CCM )akiwemo katibu wazazi na mwenezi wilaya
Wanasiasa
wametakiwa kuvusha nchi kwa Amani ikiwa ni pamoja na kuwa na uzalendo na nchin
yao,ili kuweza kulishisha kizazi kinachokuja mambo mazuri na si kuacha machafuko
kwa sababu ya uchu wa madaraka.
Kauli hiyo ilitolewa hivi
karibuni katika msikiti wa ijumaa Bakwata na Sheikh wa Wilaya ya Tarime Mkoani
Mara Sheikh Abdulhakim Mrisho Soud
kipindi akikabiddhiwa msaada wa mabati 45 yenye thamani ya shilingi laki tano
na elfu tano.
Sheikh huyo alisema kuwa
wanasiasa hawana budi kushindana kwa sera na si kushindana kwa nafsi suala
ambalo linaweza kusababisha machauko ya nchi.
“Kwa sasa haya yote
yanafanyika kwa sababu ya amani ya Tanzania machafuko yakianza kwa sababu
ya wanasiasa kizazi kinachokuja kitajifunza nini?” alisema sheikh.
Naye katibu msaidizi wa Chama
Cha Mapinuzi( CCM) Kapis Adogo kwa niaba ya mbunge wa jimbo la Tarime katika
kukabidhi msaada huo alisema kuwa viongozi hawana budi kutoa msaada bila kujali
itikadi ya vyama wala dini.
“Tutazidi kushiikiana na
viongozi wote bila kujali itikadi ya vyama wala dini lengo kubwa ni kuleta
mabadiliko katika wilaya yetu” alisema katibu msaidizi.
Kwa Upande wake katibu wa
wazazi wilaya Mathias Lugola aliwataka wazazi na walezi kulea watoto wao katika
maadili ya kidini ikiwa ni pamoja na kuendeleza mila za kiafika.
Kundi kubwa la vijana
wamebadilika hivyo wazazi hawana budi kuzidi kuwalea katika maadili ya kidini
ili kurudisha maadili alisema katibu wazazi
Naye mbunge wa jimbo la
Tarime Nyambari Nyangwine aliongea na gazeti ili kwa njia ya simu kuwa msaada
huo ni moja ya kutekeleza ahadi ambazo amehaidi katika uongozi wake.
“Nimekuwa nikitekeleza ahadi
nyingi na huo msaada wa mabati ni moja ya kutimiza ahadi zangu kama mbunge” alisema.
Nyambari aliongeza kuwa
vijana hawana budi kujishuhulisha kwa lengo la kjikwamua na si kutegemea
serikali
….Mwisho….