WAJUMBE WA KULINDA HAKI YA MTOTO WAPEWA MAFUNZO:
Picha ya mkufunzi ambaye ni Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime Mkoani Mara akitfafanua sheria ya Kulinda mtoto ni katika ukumbi wa Ofisi ya kata ya Sirari
WAJUMBE WA KULINDA HAKI YA
MTOTO WAPEWA MAFUNZO:
Wajumbe ishirini kutoka kata
ya Nyamaraga na kata ya Sirari Wilayani
Tarime mkoani Mara wmepeta mafunzo juu
ya kutambua sheria ya kumlinda mtoto ya Mwaka 2009 ikiwa ni pamoja na mafunzo
juu ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya mamana mtoto.
Mafunzo
hayo yamefadhiliwa na Shirika la Center For Children Assistance (CWCA) ambapo yamefanyika leo katika ukumbi wa ofisi
ya kata ya Sirari kwa kuhusisha wajumbe
wawili kutoka katika kata za sirari na
Nyamaraga,na vitongoji vilivyohusika ni Kitongoji cha Sokoni,kanisani,Mpakani,Buriba,Ngerengere,Remagwe,
Kitagasembe na Gwitirio lengo ni kupata elimu juu ya Sheria
ya kumlinda mtoto ya Mwaka 2009.
Kwa
Upande wake Joseph Vungwa ambaye ni Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya
Tarime ammbaye pia amekuwa mseminishaji
katika Mafunzo hayo alisema kuwa wajumbe hao hawana budi kuyafanyia kazi
mafunzo watakayo yapata kwa lengo la kuleta mabadiliko ndani ya jamii.
“Lengo
la Mafunzo ni kila mtu kuelewa sheria hii ya kulinda mtoto kwa lengo la kuleta
mabadiliko dhidi ya mtoto” alisema Vungwa.
Stephen
Ngoyani ni Mratibu wa vipindi vya kuelimisha jamii juu ya haki ya mtoto kutoka
katika shirika la Center for Widows and Children Assistance (CWCA) lililopo
Musoma Mjini ambapo makao yake makuu
yapo Dar es Salaam.
Ngoyani
alisema kuwa Shiriki hilo linajiusisha na kutoa mafunzo ya mtoto Na
21 ya Mwaka 2009, Ukatili wa
kingono kwa mtoto pamoja na uendeshaji
wa kesi za ukatili wa kingono kwa mtoto
katika Mahakama.
Aliongeza kuwa shirika hilo linayo miradi mbalimbali ikiwemo ya
kutoa usaidizi wa kisheria katika jamii, kutoa huduma ya kusomesha wanafunzi
wanaoihi katika mazingira hatarishi lengo kubwa ni kusaidia jamii.
Nao
washiriki wa mafunzo hayo walisema kuwa mafunzo hayo yawee endelevu ikiwa ni
pamoja na kufikia wahusika wote ususani maeneo ya Vijijini kwa lengo la
kufikiwa walengwa
“Wahathilika
wa matukio haya wengi wako vijijini hivyo tunaomba haya mashirika yakiwemo
mengine wawezekufika vijijini ili kutoa huduma” walisema Wajumbe.
Mafunzo
hayo yanaemndeshwa takribani siku mbili
ikiwa ni kufi ili kuweza kuelimisha
wajumbe hao kwa lengo la kuwa mabalozi kupitia vitongoji, Vijiji na Kata