Binti miaka 19 abakwa na wanaume wawili.

Binti miaka 19 abakwa na wanaume wawili.

Binti mmoja jina limeifadhiwa mkazi wa Nyamikoma kijiji cha Nyangoto  Wilayani Tarime MkoaniMara alibakwa na wanaume wawaili  huku akiwa ameshikiliwa na panga pamoja na kisu na kumusababishia maumivu makali
 
Binti huyo alisema kuwa Watu hao wawila akiwemo mme wake wa ndoa na kwa sasa ni takribani miaka mitano wameachana japo hajapewa taraka walimkuta eneo la Ofisi ya serikali ya kijiji cha nyangoto akiwa anasigina karanga za kupika ndipo walimshika  kwa nguvu wakiwa na mapanga na kupelekwa katika nyumba moja jirani na alipo kuwa akiishi hapo awali nakuanza kubakwa kwa zamu.
 
“Mme wangu anayefaamika kwa jina la Kerement Aizaki Miaka30 Mkazi wa kijiji cha kewanja Nyamongo alianza kunibaka badaea akaingia rafiki yake sikujua jina lake wakiwa wameshika mapanga na visu na badae rafiki yangu alienda akatoa taarifa kwa kaka yangu ndipo alienda polisi na kuleta polisi wakanitoa ndani majira ya saa nane mchana na akakamatwa mme wangu lakini rafiki yake alikimbia” alisema Binti huyo.
 
Chacha Masicho ni kaka yake na binti aliyefanyiwa ukatili huo alisema kuwa baada ya kupata taarifa alienda kituo cha polisi cha Nyamwaga na kutoa taarifa na ndipo polisi walielekea eneo la tukio na kukumatwa kwa mtuhumiwa huyo.
 
“Kinachozidi kunishangaza ni kwamba mtuhumiwa alipwlekwa mahakamani kwa kesi ya hapo awali kwani alishawai kumpiga mpaka akazirai lakini kesi ya ubakaji ilitupwa na amepata dhamani sasa tutafanyaje ili kumkamata iliataje rafiki yake” alisema Chacha.
 
Kaijage Kagumillwa ni mganga mkuu wa haspitali ya sungusungu iliyopo Nyamongo alisema kuwa binti huyo alipokelewa hospitalini hapo na kufanyiwa uchunguzi na kukutwa akiwa amechubuliwa sehemu zake za siri lakini hakukutwa na maambukizi yeyote na kuanzishiwa dawa za kuzuia maambukizi
 
Kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Tarime Rorya ACP Benedict Mambo sasa alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuzidi kulaani vitendo hivyo ambavyo vinatendeka
                                        ….Mwisho…
 
Powered by Blogger.