JAMII YASHAULIWA KUFUGA NYUKI
JAMII YASHAULIWA KUFUGA NYUKI
Jamii imeshauliwa kufuga
nyuki kwa ajili ya kujiingizia kipato ikiwa ni pamoja na kuongeza uchumi
wa nchi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na
Diwani wa kata ya Nyamaraga Wilayani Tarime Mkoani Mara Bw Antony Manga kipindi akiongea na Wanakikundi wa kikundi cha Ufugaji Nyuki kinachojulikanakwa jina la Twiga
Mazingira na Nyuki kilichopo kjiji cha kitagasembe kata Nyamaraga kikiwa na
wanakikundi 25 walio hai.
Diwani huyo alisema kuwa
jamii haina budi kuwekeza katika ufugaji wa Nyuki kupitia Vikundi mbalimbali ya Ujasiliamali
ili kuweza kujiongezea kipato pamoja na kuinua Uchumi wa Nchi.
“Mimi kama diwani nitazidi
kuhamasisha jamii ili kuweza kupenda kilimo cha alizeti kwa Nyumi wanapenda maua ili waweze kutengeneza Asali” alisema Antony
Christopher Momanyi ni mkazi
wa Kijiji cha Nyagisembe kata Nyamaraga na ni Mfanyabihashara katika Mji mdogo
wa Sirari ambaye pia ni Mmoja wa kikundi cha Ufugaji wa nyuki alisema kuwa
alianza kufuga Nyuki akiwa anajitegemea kuanzia Feburuari Mwaka jana na mpaka
sasaana zaxidi ya mizinga mia na ameweza kusomesha watoto kupitia Ufugaji wa
Nyuki.
“Mpaka sasa najiwekea liba ya
shilingi Elfu hamsini kwa lengo la kuendeleza ufugaji huu” alisema Momanyi.
Robi Marwa ni Mwenyekiti wa
kikundi hicha cha Ufugaji wa nyuki alizitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni
ukosefu wa Soko, Upungufu wa mizinga ya kisasa pamoja na vifaa vya kulinia
asali
Kwa Upande wake Diwani wa
kata ya Binagi Leonard Matiko alisema
kuwa ameamua kuondokana na Ufugaji wa Ngombe na Kilimo cha Kisasa kwa lengo la
kuendeleza kilimo cha Ufugaji wa Nyuki
“Baada ya kuona Mifugo
inashambuliwa na wezi nimeamua kuingia katika ufugaji wa Nyuki ambao hauna
Changamoto japo bado tunakumbwa na changamoto za ukosefu wa soko na vifaa”
alisema Diwani huyo.
…