Balozi wa papa wakristo dumisheni Upendo, Mshikamano na Amani
WAKRISTO wamewaasaa
kuheshimu na kutunza maumbile ya miili yao ambayo ni hekalu
na kuona umuhimu wake ikiwa ni sehemu ya
Uumbaji wa binadamu ili kutokwenda kinyume
na sheria ya maumbile ya Mwenyezi Mungu.
Hayo yalisemwa na Askofu Mkuu Francisco Montecillo Padilla Balozi wa Papa wa Vaticani nchini Tanzania wakati
akizungumza na wakristo wa Parokia ya Tarime katika ibada ya athimisho la kiekaristi Takatifu lilofanyika
wilayani humo.
Padilla alisema kuwa wakristo wengi wamesahau sheria ya
maumbile ya Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu ambayo ni hekalu la Mungu na
kuyaharibu pasipo kujua kuwa ni kumkosema Mungu aliyeumba maumbile hayo.
Alisema sheria hairuhusu na wanapofanya vitendo hivyo ni chukizo mbele za
Mungu na hivyo kuwaomba wawe na upendo ,amani,na mshikamano miongoni mwao na
kufuata mafundisho ya Baba Matakatifu.
Aliwasihi kuacha machafuko ya na vurugu katika makanisa ili kufanya yale
yanayompendeza Mungu kwani mafundisho ya Mungu yanapenda watu waishi kwa amani na upendo.
Aliwaomba kutumia ardhi waliyonayo vizuri kwani wamebarikiwa
sana kuliko
maeneo mengine ya nchi kwa kuwa ardhi
waliyonayo ina rutuba na maliasili nzuri
kwa ajili ya kujiletea maendeleo.
Wakati huohuo ulinzi mkali wa jeshi la polisi umeimarishwa
kila kona ya kanisa hilo
ili kuepusha mashara ambayo yanaweza kutoea katika ibada hiyo huku waumini
wakitangaziwa kuzima zima na kutofanya mawasiliano ya aina yoyote mpaka mwisho
wa ibada.
Askofu wa jimbo Katoliki la Musoma Michael Msonganzila
aliwaeleza waumini hao kuwa lengo la ziara ya Askofu mkuu ni kuleta ujumbe wa
Papa Askofu Francis wa XXVI kwa kuwaunganisha kupitia kushiriki katika ibada ya pamoja.
Msonganzila alisema kupitia ibada wanawahamasisha waumini
kuachana na mambo ya ukeketaji kwa wanawake kwa kujua madhara yanayowapata
wanawake wengi hasa wakati wa kujifungua na hata maambukizi ya magojwa mengine.