MWILI WA ALIYEKUFA KATIKA AJALI YA BUTIAMA WAFUKULI
MWILI
wa marehemu Juma Sayi mkazi wa musoma Mkoani Mara, ulikutwa umefukuliwa kaburini katika
makaburi ya Musoma Basi na watu wasiojulikana usiku wa kumkia leo.
kwa
mjibu wa taarifa za mwili huo zilizotolewa na msemaji wa familia
aliyefahamika kwa jina moja la Sayi, zlisema kuwa mwili huo ulikutwa
umefukuliwa kaburini na kukutwa nje ya kaburi hilo leo asubuhi.
Kwa
mjibu wa msemaji wa familia hiyo alisema kuwa baada ya watu hao wasio
julikana walipomaliza kuufukua na kuuweka nje ya kaburi hilo walichukua
ubao uliowekwa kaburini wakati wa mazishi hayo na kutoweka nao pasipo
julikana.
Tukio hilo liligunduliwa na ndugu
walipokwenda leo asubuhi makuburini hapo ikiwa ni siku ya tatu tangu
marehemu huyo azikwe Jumamosi, Septemba 6 mwaka huu.
''
Tulikwenda kwenye kaburi la ndugu yetu katika makaburi ya Musoma Basi
tuliko mzika kwa imani ya dini yetu ya kiislaamu na kukuta mwili wa
marehemu ukiwa umefukuliwa ndani ya kaburi lake na kukuta nje kukiwa
kumechukuliwa ubao tuliomzika nao na watu wasio julikana'' alisema Sayi.
Mara
baada ya kukuta tukio hilo walifahamisha Jeshi la Polisi chini ya
kamanda wake mkoa wa mara Phillip Karangi lililofika na kuthibitisha
tukio hilo leo.
Mwili huo ulirejea kuzikwa tena
makaburini hapo katika kaburi hilo baada ya kumalizika kufanyika
uchunguzi wa daktari na kukutwa ukiwa salama.
Tukio
hilo limedaiwa na baadhi ya watu kuhusishwa na imani ya kishirikina kwa
,kile kilichodaiwa kuwa sio kawaida marehemu mwili wake uzikwe na kisha
kufukuliwa bila utaratibu unaofahamika.
'' Sio
kawaida mwili wa marehemu kama huyu Juma Sayi, tuliyemzika hapa na baada
ya siku tatu ya leo tunakuta umefukuliwa na kuchukuliwa ubao
tuliomziika nao kaburini wanaupelekea wapi na ni kwanini waufukuwe kama
sio wachawi wanaokwennda kufanya mambo yao ya kishirkina?'',alihoji
mmoja wa wanandugu
Marehemu Juma Sayi alifariki dunia
katika ajali ya gari iliyotokea eneo la sabasaba [Songora] kitongoji cha
Irimba katika mto Rwako wilaya ya Butiama hivi septemba 5, mwaka huu
asubuhi iliyohusisha magari matatu, ya J4 EXPRESS ya aina ya YU TONG ya
usajaili T 677 CYC lilipogongana uso kwa uso na gari la MWANZA COACH
aina ya SCANIA la usajili T 368 AWJ.
Ajali hiyo
ilitokea baada ya kugongwa gari dogo la aina ya TOYOTA la usajaili T
332 AKK na basi la J4 EXPRESS lililotokea Mwanza kuelekea Sirari
[Tarime] na kuanguka chini ya daraja hilo majini wakati gari la Mwanza
Coach lilitokea Musoma lililoelekea Mwanza.
Katika
ajali hiyo watu takribani 36 walifariki dunia papo hapo na kujeruhiwa
watu 79 waliopatwa na majereha sehemu mbali mbali za mwili wake.
-----------------------------------mwisho----------