Waumini watakiwa kuondoa utafauti
Waumini watakiwa kuondoa utafauti
Waumini wa dini mbalimbali
wilayani Tarime mkoani Mara wametakiwa kuondokana na utofauti uliopo wa kidini
ili kuweza kufanikisha kazi ya bwana.
Kauli hiyo imetolewa na
Mchungaji Benjamini Daudi wa kanisa la Wadvenitist wasababato mjini kati
lililopo wilayani Tarime kipindi akitoa neno la bwana kuhusu changizo la
harambee iliyoandaliwa na kanisa hilo kwa lengo la ujenzi na upanuzi wa kanisa.
Mchungaji huyo alisema kuwa
waumini hao hawana budi kuhakikisha wanamtolea mwenyezi mungu matoleo ya
kumpendeza ili kuweza kunyoshewa njia katika
utendaji kazi wao na kuondokana na mitafaruko kwa baadhi ya waumini.
“Kazi ya mwenyezi mungu ni kubwa hivyo waumini wote
tunganishe nguvu ya pamoja kwa kuharikana ili kufanikisha lengo la upanuzi wa
kanisa” alisema mchungaji.
Ilisemwa kuwa zaidi ya watoto
mianane wamekuwa wakisalia nje kwa sababu ya ufinyo wa kanisa hilo suala ambalolimepelekea kuandaa harambee
hiyo kwa lengo la kupanuajengo ili
wahumini wote waweze kusalia ndani ili kupata neno la bwana kwa pamoja.
Katika harambee hiyo mgeni
rasimi alikuwa mwenyekiti wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa mara Bi: Nancy
Msafiri amabapo alisema kuwa ujenzi wa nyumba ya bwana ni jukumu la kila
muhumini ili kuweza kupata baraka kutoka kwa mwenyezi mungu.
Mgeni rasmi aliongeza kuwa
umoja, Upendo na Mshikamano ni nguvu ya mwenyezi munguhivyo vyote kwa pamoja na kupaza sauti moja mwenyezi mungu
usikia na kutoa nguvu ili kufanya kazi iliyokiusudiwa.
“Nafasi tuliyonayo sisi watu
wamungu tunabidi kuitumia vizuri ili kumpendezesha mwenyezi mungu” alisema
mgeni rasimi.
Hata hivyo mgeni rasmi alisema
kuwa lengo la harambee hiyo ilikuwa ni kupata shilingi millioni miamoja ambapo
wamepata zaidi ya millioni arobaini na sita
ikiwa ni jumla ya michango yote ikiwemo ahadi ya millioni kumi na nne ,
Vifaa mbalimbali vya ujenzi na thamani
ya vitu vilivyotolewa katika harambee hiyo.
Kwa upande wake mzee wa
kanisa kiongozi Joshua Marwa alitumia fursa hiyo kutoa shukrani za dhati kwa
waumini waliofanikisha lengo hilo
la changizo la harambee ya ujenzi wa nyumba ya bwana.
Kwa niaba ya waumini wa
kanisa la Tarime kati la wadventist wasabato natoa shukrani mungu awabaliki na
mzidi kuyonesha moyo wa upendo na umoja wenu katika kumchangia mwenywzi mungu”
alisema mzee wa kanisa.
…………Mwisho…