Wanne wauwawa katika kata ya Muriba nane mbaroni.
Wanne wauwawa katika kata ya Muriba nane mbaroni.
Katika kijiji cha Muriba kata
ya Muriba Tarafa ya Ingwe wilayani Tarime Mkoani Mara Mnamo 8 Agosti Mwaka huu majira ya saa tatu usiku watu wane walisadikiwa kuwa ni majambazi raia
wa nchi jirani ya kenya
waliuwawa.
Kwa mujibu wa kamanda wa
polisi katika mkoa wa kipolisi Tarime Rorya ACP Lazaro Mambosasa alisema
kuwa watu hapo walitambuliwa mmnamo
Agosti 03 mwaka huu majambazi hao waliweza kuvamia kijijini hapo wakiwa na silaha za kivita na mapanga na
kufanikiwa kupora fedha dukani kwa mfanyabihashara aitwaye Shadrack Mahenya
ambaye ni mmiliki wa duka la jumla na rejareja kijijini hapo na watu watu
walijeruhiwa katika tukio hilo.
Kwa mujibu wa kamanda huyo baada ya wananchi
kutambaua miongoni mwa majambazi hao waliofanya uvamizi wa tukio hilo kutoka
katika kijijihichobhabada ya kuzuka taharuki
kubwa iliyokuwa bado inatenda
miongoni mwa wananchihao na ndipo kundi la wananchi lilijitokeza
nakuwazidi viongozi wa serikali nguvua na kuanza kushambulia watuhumiwa baada
ya kuhojiwa na kukiri kuwa walishiriki katika unyanganyi huo.
Kamanda aliwataja kwa majina
kuwa marehemu walitambulika kwa majina ya Sagire Magasi Mkurya 25 mkazi wa Mfanya mfanya
bihashara wa kuhuza supu nchini Kenya,na ni mkazi wa kijiji cha itilio wilayani
Tarime wa pili ni Mwita Rugema mkurya 30 mkulima na mkzai wa ntimaru Kenya wa
tatu Rogna Nyamoahoyi mkulima kazi wa Kenya, Machera Sando Marwa mkurya mkulima
wa Girabose nchini Kenya.
Chanzo cha tukio hilo la
mauaji ni taarifa ni taarifa zilizopokelewa hapo kijijini zikieleza kuwa
watuhumiwa hao ni majambazi na kwamba waliousika mnamo agosti 3 mwaka huu
tukioambalo lilitokea kijijini hapo na kusababisha majeruhi watatuna kuwapora
fedha na jeshi la polisi walipopata taarifa walifanya juhudi za kuokoa
watuhumiwa hao sauala ambalohalikuzaa matunda na miili imeifadhiwa hospitali ya
halmashauri ya mji wa Tarime huku zikisubiliwa juhudi za mazishi.
Mpaka sasa jeshi la polisi
kanda maalumu Tarime Rorya kwa ushirikiano wa kamishena msadizi wa jeshi la
polisi watu nane wanashikiliwa kwa maho jiano
zaidi na watu hao ni Modesta Ghati 40 kurya,Mofati Mwita 50 kurya,Mhina chacha
26 kurya, Mwita wambura 46, Nyamuhanga
Mwita42, Samweli Nyagisare Chacha 25 na
James Chacha 50 wote wakurya.
Kamanda ametoa wito kuwa
jamii iondokane na suala lakujichukulia sheria mkononi bali itoe taarifa kwa
jeshi la polisi pale inapobaini mwalifu.
…..MWISHO….