Mchungaji azidi kukemea vitendo vya ukatili
Mchungaji azidi kukemea vitendo vya ukatili
Mchungaji wa kanisa la
Evanjeristi Assembly of god Thomas Rioba amezidi kukemea vitendo vya ukatili wa
kijnsia dhidi ya mama na mtoto ambavyo vimekuwa tishio kubwa vinavyozidi kutendeka
katika jamii wilayani hapa vikiwemo vya kuchomwa kwa moto, kuawa na kutolewa
kwa baadhi ya viungo vya binadamu pamoja na kujeruhi kwa mapanga waweze kubadilika ikiwa ni pamoja na
kuondokana na mitazamo hasi ili kuweza kumrudia mwenyezi mungu.
Mchungaji huyo alizidi
kuitaka jamii ya kikurya kuondokana na mila potofu ambazo zinazidi kukandamiza mtoto wa kike na kumukosesha haki zake za msingi kama vile Elimu.
“Tumekuwa tukishudia matukio
mbalimbali wanayotendewa ndugu zetu hivyo tufikie hatua na kumwogopa mwenyezi
mungu ili kutangaza wilaya yetu kwa mazuri” alisema mchungaji huyo.
Naye mkurugenzi mtendaji wa haki za binadamu
wilayaniTarime Mkoani Mara (SHEHABITA) Bonny Matto ameitaka jamii kuondokana na suala zima la kujichukulia
sheria mkononi ikiwa ni pamoja na kufuata sheria zilizopo ili kuishi kwa amani.
Aliongeza kuwa suala la
kukiuka sheria ndo chanzo kikubwa na kisababishi cha uvunjifu wa amani ambao
unasababisha vitendo vya ukatili wilayani hapa.
“Jamii kwanza ibadilike ili
tuweze kutokomeza vitendo vya ukatili iliwa ni opamoja na wazazina walezi
kukubali mabadiliko kwa sasa
tumezanzisha mafunzo juu ya athali za ukatili katika wilaya ya Tarime na Rorya
ili kutokomeza vitendo hivi” alisema Mkurugenzi.
Kwa upoande wake mratibu wa
shirika la jukwaa la Mtoto (CDF) Restuta mpate aliwaomba wazee wa kimira pamoja
na viongozi wa serikali za vijiji
kuungana pamoja ili kutokomeza vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa endapoa jamii
ya vijiji ikiondokana na ukimya itasaidia kupunguza vitendo hivyo vya ukatili
na kuweza kubaini watuhumiwa wa vitendo hivyo ili kuchukuliwa hatua za
kisheria.
Kwa upande wake mkurugenzi wa
chama cha waandishi wa habari wanawake (Tamwa) Valerie Msoka amezidi kukemea
vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyozidi kutokea wilayani humo.
“Jamii iondokane na mambo ya
kumnyanyasa mtoto wa kike pamoja na
udhalilishaji ili mwanamke hawreze kuijikomboa tunaendelea kutoa elimu kwa
vyombo vya habari ili vizidi kupaza sauti kwa lengo la kukomboa mwanamke” alisema.
Sanjari na hayo serikali kupitia
halmashauri za Wilaya ya Tarime na Mji wa Tarime hawana budi kuhunda mbinu
mbadala ili kukomesha vitendo vya ukatili wilayani humo.