Madiwani wachachamaa kudai waraka ili kupata viko vitatu

 
Madiwani wachachamaa kudai  waraka ili kupata viko vitatu

   
MKURUGENZI wa halmashauri ya Mji wa Tarime Venance Mwamengo hivi karibuni amekwepa rungu la Madiwa wa halmashauri hiyo kumtaka kufanya vikao 3 vya Baraza badala ya vikao 2 kwa sasa swali ambalo liliibuliwa na Diwani kata ya Sabasaba Chirstoph Chomete.
 
Aidha Mkurugenzi huyo alidai mbele ya baraza la madiwani kilicho fanyikia uwanja wa halmashauri Agost,01,2014 na kusema kuwa hajapokea Waraka wowote kutoka Serikalini ambao unamruhusu kufanya vikao vya Baraza 3 badala ya 2 kwa sasa na kuwa kufanya hivyo atakuwa amegeuka maadili ya kazi.
 
''Hapa kwetu tunafanya kikao cha Chama na kikao cha Baraza la madiwani lakini kikao cha Madiwani kuwasilisha hali ya maendeleo ya kata yake hatufanyi kwa sababu hatuja pokea Waraka wowote amabo unaniruhusu na nikipata waraka hiyo haina shida''alisema Mwamengo.
 
Majibu hayo yalizua mtafaruku katika kikao hicho ambapo madiwani walitaka kujua sababu ya kushindwa kufuatilia waraka hata katika halmashauri zingine kama vile halmashauri ya Tarime iliyo karibu na kuendana na wakati.
 
Akifafanua Chomete alisema kuwa kuna haja halimashauri yake kuiga kutoka halmashauri zingi ambazo zinaendesha vikao 3 badala ya 2 kama waraka unavyosema na kuongeza kuwa Mkurugenzi asiendelee kung'ang'ania mfumo wa zamani ambao umepitwa na wakati badala yake atafute waraka kutoka halimashauri zingine ambazo tayari zimekwisha upata.
 
Chomete alitaja Halmashauri amabazo tarari zimeingia katika mfumo wa kufanya kikao 3 badala ya 2 kama ilivyo kuwa hapo nyuma kuwa ni pamoja na halmashauri ya Tarime,halmashauri ya Serengeti na hata halmashauri ya Musoma na kuwa Mkurugenzi atafute waraka huo katika halmashauri hizo.
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Daudi Wangwe aliwatuliza madiwani na kudai kuwa atahakikisha analivalia njuga swala hilo na kuwa wanapata waraka ambao utawaruhusu kuendelea kufanya vikao 3 kama halmashauri zingine.
 
''Hata mimi nina haja ya kuwasilisha hali ya maendeleo ya kata yangu katika baraza hili lakini kutokana na kuwa hatuja pokea Waraka wowote ambao Unaturuhusu kufanya vikao 3 hatutalazimisha kufanya bila kuwa waraka kwa hali hiyo tuendelee kuwa watulivu wakati hatua zingine zinaendelea kufanyika na kuhakikisha kuwa tunaingia mfumo mpya wa vikao''alisema Wangwe. 
........................................................mwisho.....
Powered by Blogger.