Wananchi tunzeni vizuri Mira
Picha
ya mwenyekiti wa kijiji cha Nyamwaga Tarafa Ingwe Mkoani Mara ambaye
pia ni katibu wa Ushirika wa Nyabigena Security Mining Cooperative
uliopo Nyamwaga akifafanua jinsi wananchi wanavyonufaika na Misaada
kutoka Mgodi wa dhahabu wa Nyamongo African Barrick Gold Mine(
ABG)
Wanachiwametakiwa kutunza
miradi wanaopewa ili miradi hiyo iweze kutumiwa na kizazi kianchokuja pamoja na kunufaika kupitia Miradi hyo
Kauli hio imetolewa na
Mwekiti wa kijiji cha Nyamwaga ambaye pia ni katibu wa Nyabigena Saccos Mining Security Cooperative Kirigiti Sasi iliyopo Nyamwaga Tarafa ya Ingwe Wilayani
Tarime Mkoani Mara.
Mwenekiti huyo alitoa kauli hiyo kipindi akiongea na gazeti ili
kuhusiana na vijiji vinavozunguka mgodi wa African Barrick Gold Mine (ABG) North Mara ulipo Nyamongo vinanufaika vipi na
je miradi wanayopewa wananchi wanailinda vipi ili isiweze kuharibika.
Alisema kuuwa mgodi huo
umekuwa ukitoa misaada mbalimbali na
vikundi mbalimbali pamoja na ushirika ambao unatambulika Serikalini kwa
lengo la kuleta maendeleo katika vijiji saba vinavozunguka mgodi huo lakini
wananchi waliowengi wamekuwa wakitunza miradi hiyo japo changamoto zipo.
Aidha Kirigiti alisema kuwa
kupipia Ushirika wao wamekuwa wakipata
ufadhili wa mgodi na kuweza kuwapa kazi mbalimbali ndani ya Mgodi na nje ya
Mgodi ili vijana wanaozunguka vijiji saba waweze kupata ajila kupitia ushirika
huo na kusema Ushirika huo unajumla ya wafanyakazi 917 ambao wameweza kupata
ajila kupitia Miradi mbalimbali inaoendeshwa na Ushirika huo wa Nyabigena huku Ushirika wa Saccos ukiwa na Wafanyakazi,
122, 300 walinzi na140 wakifanya Sido kazi mbalimbali kupitia uhirika huo na Sido
Wafanyakazi 80.
Pia aliongeza kuwa mapa ka
sasa ushirika wao wa Kuweka na kuko kwa sasa una jumla ya zaidi ya Millioni 200 na kusema kuwaUshirika huo umekaguliwa na msajili
wa vyama vya Ushirika Mkoa a wa Mara, na
kila mwanachama ana uwezo wa kukopa ili kuweza kufanya mairadi yake ya msingi
pamoja na kusomesha watoto.
“Tunazidi kushukuru Mgodi wa
Barrick umetusaidia misaada mbalimbali, tumepewa tenda za usafi, Kukusanya
vyuma chakavu,na kupulizia dawa ya mbu ili kuwakinga na maralia wafanyakazi wa
mgodini na tunapata kipato” aliseama.
Sanajari na hayo katibu huyo
wa Ushirika alisema kuwa kupitia miradi wanayopata vijana kutoka Moshi, Mwanza
wameweza kupta ajila pamoja na vijana wanaozunguka mgodi huo wa Nyamongo.
“Ninapata maendeleo kawa
sababu nashirikisha wananchi wangu na kutoa maamuzi nawaomba viongozi wenzangu
waondokane na siasa katika masuala ya Maendeleo kwani mgodi una nia nzuri ya
kutusaidia na unazudi kutekeleza miradi ya jamii kulingana na miktaba ya vijiji
inavyosema” alisema.
Licha ya hayo alisema kuwa
kupitia ushirika huo wameweza kulipia watoto wanaishi katika mazingira magumu
pamoja na ulemavu ambapo kwa wasasa wanatarajia kuomba mgodi ili waweze kujenga
nyumba za kisasa sitini ili waweze kukodisha mgodi ili wafanyakazi wa mgodini
waweze kutumia makazi hayo.
“Tunatarajia kuongea na Meneja wa mgodi tuweze kupewa hiyo
tenda na mpaka sasa tayari tumejenga nyumba moja ya mfano iliaje akague na
kulidhia tuweze kujenga nyingine ili ushirika ukakauwe mwisho kuwa banki”
alisema.
…….
Mwisho….