Polisi fc walazwa kwa kichapo cha bao 2-1 didi ya Mafundi fc:
Picha ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Tarime rorya SACP
Justus kamugisha kulia akikabidhi kaputeni wa timu ya mafundi Fc Babu
Matacha ngao ya ushindi baada ya kukabidhiwa zawadi ya shilingi laki
moja baada ya kuilaza polisi fc Tarime kichapo cha bao 2-1 katika uwanja
wa serengeti Mjini Tarime
Timu ya polisi Fc Tarime
imelazwa kichapo cha bao 2-1 dhiodi ya Mafundi Fc Tarime katika michuano ya
kumwaga aliekuwa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Tarime Rora SACP
Justus Kamugisha katika viwanja va Serengeti Mjin Tarime.
Katika mashindano hayo ambayo
yamewakutanisha watani wa jadi hao wawili kipindi cha kwanza mchezo huo waliweza kutoana jasho
mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika walitoka bila ya kufungana na ndipo
kipindi cha pili dk ya nne Mfundi fc walichungulia nyavu za polisi fc kupitia
kwa Barnabas Wilibard na kudumu mpa dakika ya
72 ndipo polisi fc kupitia kwa Godfrey
Francis alisawazisha.
Mtanange huo ulizidi kutoana
jasho ndipo kipindi cha dk 76 Thomas
Marwa alipachika bao na kusababishia mafundi kujinyakulia ushindi huo.
Katika Mashindano hayo
mshindi wa kwanza ambaye ni Mafundi Fc walipewa zawdi ya shilingi, 100,000 na
Ngao ya Ushidi na mshibdi wa pili Shilingi 50,000.
Kwa upande wake kamanda wa
jeshi la polisi Mkoa wa kipolisi ambaye kwa sasa amehamishiwa mkoani shinyanga
aliwataka wanamichezo hao pamoja na wadau wa michezo kuzidi kudumisha michezo
wilayani Tarime pamoja nakutoa Ushirikiano wa kutosha kwa kamanda mpya ili
kuboresha soka wilayani Tarime.
“Nitaendelea kuwasaidia
katika michezo lakini kuweni na
Ushirikiano wa kutosha” alisema kamanda.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha
Mpira willaya TAFA John Rutente aliwaimiza wachezaji hao kuendeleza soka ili
kuweza kuibua vipaji vya kutosha ndini ya wilaya.
“Vipaji tunavyo vya kutosha
kikubwa ni kuzidi kuwekeza katika suala zima la soka wilayani hapa” alisema
Mwenyekiti Tafa.
…….MWISHO….