Wakina mama watakiwa kuwa na maamuzi ya dhati
Picha
ya mbunge wa viti maalumu jimbo la Tarime Ester Matiko akiongea na
waandishi wa habari pamoja na wananchi mbele ya ofisi za chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema)baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti
wa akina Mama Mkoa wa Mara katika chaguzi zilizokuwa zikifanyika Musoma
mkoani Mara ili kupata viongozi katika ngazi mbalimbali kulia kwake ni
katibu wa mkoa wa Mara aliyechaguliwa katika chaguzi hizo Mwl Chacha
Heche.
Wakina mama wametakiwa kuwa
na maamuzi ya dhati katika nyakati za uchaguzi ili kuweza kuwapata viongozi
waadilifu na wa kuleta mabadiliko katika jamii.
Kauli hiyo ilitolewa jana na
Mbune wa viti maalumu kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Bi: Ester Matiko kipindi akiongea na gazeti ili baada ya ushindi wa
kuwania kiti cha mwenyekiti wa akina mama mkoa wa Mara katika chaguzi
zilizokuwa zikifanyika hapo juzi mjini musoma mkoani Mara ili kuweza kuwapata
viongozi katika nyadhifa mbalimbali kupitia ngazi ya Mkoa.
Mbunge alisema kuwa wanawake
hao hawana budi kuondokana na zawadi ndogondogo
zinazotolewa na wagombea katika nyanja mbalimbali bali waunganishe nguvu
ya pamoja ili kuweza kujikwamua na kufanya mapinduzi katika uongozi.
“ Nimechaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa akina mama mkoa wa Mara hivyo naitaji nguvu kubwa na ushirikiano
kwa akina mama ili tuweze kujikwamua” alisema
mbunge.
Aidha mbune huyo alisema kuwa
atatumia fursa aliyonayo kuwahamasisha wakina mama ili kujiunga na vikundi huku
wakianzisha ujasiliamali kwa lengo la kujikwamua katika uchumi.
“Wanatarime ni wakati maalumu
kushirikiana na viongozi ili kuweza kufanya mapinduzi na kujenga jimbo
letu huku tukikemea makundi yanayoanzishwa hapa” alisema.
Kwa upande wake katibu wa
chama hicho Mwl Chacha Heche alisema kuwa katika utendaji wake wa kazi ataweza
kushirkisha viongozi wote wazee ili kuweza kushauri chama hicho na kuondoa
tofauti ndani ya wilaya zote zilizopo ndani ya mkoa wa Mara.
Hata hivyo katibu aliongeza kuwa makundi hayatakifikisha
popote chama hicho bali vionozi wote waunganishe nguvu ya pamoja ili kuweza
kukitangaza chama hicho upya wilayani Tarime.
Nia tunayo sisi bado ni
wazalendo nia yetu ni kusikiliza wananchi na kufanya mambo ya maendeleo alisema
katibu huyo.
…..Mwisho….