Kopa kokakola wachagua vipaji Tarime.
Kopa kokakola wachagua vipaji Tarime.
WACHEZAJI ambao walishiriki Ligi ya Kopa kokakola Wilayani Tarime Mkoani Mara juzi katika viwanja vya Sereneti mjini Tarime
wamlitimua vumbi ili kuwasaka vijana wenye vipaji kwa lengo la kuunda timu ya
mkoa hadi Taifa.
Wachezaji hao wametoka katika timu mbalimbali zilizopo ndani
ya wilaya ikiwamo timu ya mpira wa miguu Buhemba Kids,Rebu shule ya
msingi,Sirari Kids,Tarime Kids,Mafundi KidsTarime United pamoja na Tadea Kids
walijikuta amabapo wamejikuta wakimaliza mchuano huo kwa mazingira magumu bila
chakula na badala yake wameambulia kushindia maji ya kama chakula cha mchana
kwani mechi hizo zilianza majira ya asubuhi msaada huo ulitolewa na na Mbunge
wa viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Estar
Matiko
Ligi hiyo ilianzishwa na Shirikisho
la Mpira Duniani FIFA chini ya udhamini wa kopa kokakola kwa lengo la kuibua
vipaji.
Akizungumza juzi Kocha wa
Mkoa Mara James George juu ya mchuano huo alisema kuwa kanuni za kopa kokakola
ni kunyanyua soka na kusaka vipaji.
‘’Lengo ni kuwapata wachezaji
20 kutoka Wilaya Tarime ambao watakwenda kuunda Timu ya Mkoa 20 kanda na
hatimaye timu ya Taifa na hapa hatuhitaji mshindi badala yake tunasaka wenye
vipaji na kuteneneza safu nzuri’’alisema George.
Aidha aliwataja
waliochaguliwa kwenda kuunda Timu ya Mkoa kuwa ni paja na Willbardi
Pastori,Ayubu Joseph,Justin Morisi,Charles Chacha kutoka timu ya Rebu,Makori
Baraka,Maambo Wanzagi Bonfasi Clofas wote kutoka Buhemba Kids,Mokami
Issa,Joseph Chacha kutoka Sirari.
Wengine ni pamoja na Maiko
Selevestar Erick Eriuta,Charles Thobias,Hashimu WatororoMwita Kisyeri,Yahaya
Forouk,Dishoni Chomete wakutoka Mafundi na Omari Anderea TevienMatacha wa
Tarikme United kukamilishan idadi ya wachezaji 20 kutoka Tarime kuwakilisha
Mkoa.
Kwa upande wake Moja wa
wajumbe wa kamati tendaji Gabriel Gweso Nyagesagane alisema kuwa Timu nyingi
hazikushiriki lii hiyo kutokana na mazinira magumu ya kufika eneo la tukio
sanjari na ukosefu wa usafiri.
Aidha Nyaesagane aliongeza
kuwa wachezaji wamekoswa chakula kutokana na mdhamini kushindwa kuwaandalia
wachezaji bajeti ambayo inakidhi mahitaji.
Aidha timu ya wachezaji
wengine wameshindwa kuhudhuria kushiriki ligi ya kopa kokakola kutokana na
nauli,vifaa vya michezo na mahitaji mengine ambapo mfadhili anatakiwa kutoa
kabla katika viongozi wa chama cha mpira kila Wilaya.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,mwisho,,,,,,,,,,,,,