Madiwani tumieni vizuri fedha kukamilisha miradi
Madiwani wilayani Tarime
mkoani Mara wametakiwa kutumia vizuri fedha za miradi mbalimbali ili kuweza kukamilisha miradi huska kwa lengo
la kusukuma gurudumu la maendeleo katika kata.
Kauli hyo ilitolewa jana na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya
ya Tarime amabaye pia ni diwani wa kata ya Sirari Amos Sagara katika balaza la
kawaida la madiwani lililofanyika katika
ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti alisema kuwa
madiwani hao hawana budi kutumia fedha hizo katika miradi huska ili iweze
kumalizika haraka miradi huyo na kuondoa
migogoro inayojitokeza baada ya miradi kutomalizika kwa muda mwafaka.
“Tukianza na fedha ambazo
tulipewa na mgodi wa dhahabu wa African Barrick Gold Mine (ABG) uliopo Nyamongo
wilayni Tarime Mkoani Mara dola laki nane na kutenga kila kata shilingi
Millioni30 kwa kila kata hivyo madiwani walichagua miradi ambayo itatekelezwa
sasa tumieni fedha hizo vizuri” alisema Mwenyekiti.
Hata hivyo Sagara alisema
kuwa kupitia halmshauri hiyo walitoa kipaumbele suala la Afya na Elimu katika
fedha hizo ambazo ziligawiwa na badae madiwani walirudi na kuomba miradi
mingine kama vile barabara.
“Kulingana na miradi ambayo
mmeomba nyie Madiwa itimizeni kwa wakati” alisema.
Sanjari na hayo mwenyekiti
amekemea baadhi ya wakandalasi wanapata tenda za Halmashauri ya Wilaya ya
Tarime na kutozikamilisha kwa muda mwafaka.
Madiwani kupitia baraza ili
pitisheni ili watu kama hao wakirudi wasipate
kwa sasa wanachelewesha maendeleoya wananchi alisema.
…..Mwisho….