Shule ya msingi Michire yakumbwa na uhaba wa madawati na Vyoo.
Picha ya Mbunge wa viti maalumu Estre Matiko kulia akihesabu fedha shilingi laki tano kwa ajili ya kumkabidhi diwani wa katoa ya Mukoma Kitori lazaro kwa ajili ya ujenzi wa choo katika shule ya msingi Michiri iliyopo wilayani Rorya Mkoani Mara
Shule ya Msingi Michire
iliyopo Rorya Mkoani Mara inakumbwa na uhaba wa madawati na vyoo suala ambalo
linapelekea wanafunzi 46 kutumia Madawati 9 katika darasa moja shuleni hapo.
Mwalimu mkuu msaidizi katika
shule hiyo Mwl Elias Masatu alisema kuwa shule hiyo inakumbwa na changamoto
hiyo ya uhaba wa madawati, Vyoo poamoja na
Nyumba za walimu.
“Shule yangu inajumla ya
wanafunzi 373 ina matundu ya vyoo 12 wasichana Matundu 6na wavulana 6 lakini
tunaekea kipindi cha mvua vitajaa na kupelekea shule kufungwa” alisema.
Sanjari na ukosefu wa nyumba
za walimu zipo baadhi ya nyumba ambazo kwa sasa zina zaidi ya miaka 20 hazijakamilika
kwa sababu ya migongano ya vyama vya kisiasa sula ambalo linarudisha maendeleo
ya wananchi katika kata hiyo.
Kwa upande wake Diwani wa
kata ya Mukoma wilayni humo Kitori lazaro alisema kuwa uhaba wa madawati katika
shule hiyo ni chanamotokubwa sana.
“Katika wilaya yetu tunajumla
ya shule 119 na uhaba wa madawati 9720 suala ambalo linapelekea asilimia kubwa ya wanafunzi katika shule za
msingi kukaa chini” alisema diwani huyo.
Naye Mbunge wa viti maalumu
kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Tarime
Bi:Ester Matiko alitoa shilingi laki tano kwa lengo la kuchangia ujenzi wa choo
unaoendelea shuleni hapo.
“Mwaka jana nilialikwa kuja
kuwa mgeni rasmi lakini sikupata nafasi ya
kufika hivyo sasa natoa hizi fedha kama
mama mzazi ili kunusuru watoto wetu waendelee na masomo shule isifunwa kwa
sababu ya choo” alisema.
Hata hivyo Katibu wa chama
hicho Mkoa wa Mara Mwl Chacha Heche alisema kuwa ni moja ya kuanzi katika
utendaji kazi wake na kuwataka viongozi kuonesha kazi kwa vitendo na kuondoa
tofauti za vyama ili kusukuma urudumu la Maendeleo ndani ya Mkoa wa Mara.
“Lengo kubwa ni kuwa na
Maendeleo ndani ya mkoa wa Mara na si kukaa ,makundi kujadili itikadi za vyama
haimusaidii mwananchi wa kawaida” alisema katibu wa mkoa
…..Mwisho….
…..Mwisho….