Mjamzito na mume wakatwa mikono ya shoto

Mjamzito na mume wakatwa mikono ya shoto


Mjamzito na  mume wakatwa mikono ya shoto

Magori chacha (23) na mke wake Rahel Magori (21) wakazi wa kijiji cha
Nyarwana kata ya Kibasuka Wilayani Tarime wote kwa pamoja wamepoteza
mikono yao ya kushoto kwa kukatwa na watu wasiofahamika  na
kusabaishiwa kilema cha maisha.
Tukio hilo linadaiwa kutokea Agosti 28 saa tano usiku wakati  watu
wawili ambao walikuwa wamevaa nguo zisizoonyesha sura zao wakipoingia
ndani ya nyumba na kuwakuta Chacha na mkewake  wote wawili wakiwa
wamelala na kuanza kuwakata kwa panga huku wakiwajeruhi upande wa
kushoto wa mili yao wote.
Wakisimulia tukio lilivyokuwa Chacha akiwa katika  wodi namba tatu
katika hospitali ya halmasauri  ya mji wa Tarime, alisema kuwa usiku
huo wa Agosti 28 majira ya saa tano wakiwa wamelala walisikia watu
wakivunja mlango kwa nguvu na kuingia ndani huku wakiwa wamewasha
kurunzi kisha kuanza kuwakata kwa mapanga.
“Nilishitukia mlango unafunguliwa maana haufungwi kwa komeo,
tunaufungia kipande cha mti kwa kuegesha, wakiwa wamevalia nguo
zilizofunika nuso zao bila kusema lolote kila mwingine akamkata mke
wangu mkono wa kushoto karibia na bega name mwingine akanikata mkono
huohuo karibu na kiwiko yote ikakatika na kuanguka chini” alisema
Chacha.
Akaendelea kusimulia “tukapiga yowe usiku huo watu wakaja wakatuchukua
hadi kituo cha afya Sungusungu Nyamongo hali ikashindikana madakidari
wakachukua gari kutuleta hapa usiku huohuo na sasa tunaendelea na
matibabu ila maumivu ni makali” alisema.
Akiwa katika wodi namba sita Rahel Magori alisema kuwa tangu aolewe
haja maliza mwaka na hajuli llolote lililosababisha watendewe unyama
huo kwa kuwa kwa muda wote tangu aolewe hapo hajawahi kusikia mume
wake akishutumiwa na jirana ama ndugu yeyote.
“Sijapata mtoto ndio nina ujauzito wa miezi ninane na nusu, ikiwa
walikuwa na ugomvi na mume wangu wangemjeruhi tu na kumwacha, sasa
mimi naye nilikuwa nimewakosea nini hadi wanikate mkono wangu?
Namwomba tu Mungu anisaidie nipone”alisema Magori huku machozi
yakidondoka kitandani alikokuwa amelazwa huku akiwa ametundikiwa chupa
ya damu.
Hata hivyo awali Chacha alisimulia kuwa aliwahi kuwa na ugomvi na baba
yake mdogo aliyemtaja kwa jina la Mgesi Nkombe kuwa mwaka 2012 aliwahi
kuvamiwa lakini akadai kuwa anawajuwa waliohusika kwenye uvamizi huo,
na kati ya waliowekwa chini ya ulinzi alikuwa yeye.
Hata hivyo alikaa gerezani miezi mitano kisha kuachiwa huru baada ya
ushahidi kukosekana kuonyesha kuwa alikuwa ni mhusika lakini
aliendelea kutishiwa na baba yake kuwa adhabu yake bado.
“Baada ya kuachiwa huru kutokana na baba mdogo kushindwa kuleta
ushahidi wa mimi kumvamia, alinitamkia kuwa mimi bado na viongozi wote
wa kijijini kwetu wanataarifa hizo za kunitishia” alisema chacha.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Bernard Makonyo alisema kuwa wakati
wamawapokea meruhi hao walikuwa katika hali mbaya kutokana na majeraha
waliyokuwa nayo lakini walipopata huduma ua kushonwa , kuongezewa maji
na damu wanaendelea vizuri licha ya maumivu wanayoyapata kutokana na
kupoteza sehemu za mikono yao.
“Tuliwapokea saa 9 usiku wa kuamkia Agosti 29 wakiwa katika hali mbaya
baada ya hali hiyo kushindikana kule Sungusungu Nyamongo na kuamua
kuwaleta hapa licha ya kukatwa mikono ya kulshoto wote wawili lakini
pia wamejeruhia sehemu za paja la shoto wote na miguu kwa panga”
alisema Dr. Makonyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi wa Tarime Rorya kamishina msaidizi
Lazaro Mambosasa alikiri kuwa na taarifa ya tukio hilo na kuwa hakuna
mtu aliyetiwa hatiani, majeruhi walikuwa hawajapata nafasi ya kutoa
malezo polisi kutokana na hali zao zilivyokuwa na kuwa litafanyiwa
kazi” alisema Mambosasa.
mwisho
Powered by Blogger.