Serikali isikie kiliochetu Walemavu;
Katibu wa chama cha walemavu Bw:
Robart Masunga ameiomba Serikali kutoa kipaumbele kwa watuwanaoishi na ulemvu
ili kuweza kuijikomboa kiuchumi, kisiasa na kitamaduni kwani wamesaurika .
Katibu huyo ametoa kauli hiyo jana
kipindi akiongea na gazeti hili kuhusu mpango ambao anategemea kuanzisha kwa
lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii ili walemavu hao waweze kusaidiwa
Alisema kuwa wanampango wa kuzunguka
katika kata saba huku wakifanya midaharo mbalimbali na kuelimisha walemavu
kuhusu haki zao kwa lengo la kuwafumbua macho.
“Nia yetu kubwa ni kuzungunguka
Maeneo ya vijijini kwani takwimu kubwa ya walemavu hawajapata Elimu kuhusu haki
zao za msingi na Serikali imetusahau japo Mashirika mbalimbali ndo yanazidi
kutupa vipaumbele” alisema Katibu huyo.
Aidha Bw: Robert alisema kuwa
wanafunzi kutoka katika vyuo mbalimbli hapa nchini wamekuwa wakiwasilisha
matatizo yao ili waweze kusaidiwa kupitia chama hicho lakini wanakwama kwa
sababu mfuko wao hauna pesa za kiutosha.
“Tuna mpango wa kuomba msaada
kupitia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Venance Mwamengo pamoja na
Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Athuman Akalama na Mbunge wa Jimboletu waweze
kutusaidia ii kutunisha mfuko wetu na kufanikisha lengo letu la ziara ya
mafunzo kwa walemavu ususani maeneo ya vijijini” alisema.
Hata hivyo Katibu huyo aliongeza
kuwa baada ya Halmasgauri kuwa mbili kuna haja ya kusajiri chama cha walemavu
kupitia Halmashauri ya Mji wa Tarime baada ya kuzaliwa kutoka Halmashauri
yaWilaya ya Tarime ili kiweze kupewa kipaummbele katika kupata Misaada kama
vyama vingine hapa nchini.
Mwisho amezidi kutoa kili hata kwa
mashirika mbalimbali yenye kutetea haki za walemavu kuzidi kupaza sauti ili
serikali kusikia kilio chao ususani kwa sasa katikamchakato wa kutafta katiba
Mpya.