Wananchi waunganisha nguvu kudai fidia Maeneo yaliyofanyiwa Uthamini na Serikali:
Wananchi waunganisha
nguvu kudai fidia Maeneo yaliyofanyiwa Uthamini na Serikali:
Tarime:
WANANCHI wavijiji saba vinavyozunguka Mgodi wa Afrika
Barrick Gold Mine wameungana pamoja katika swala zima la kudai fidia maeneo yote
ambayo yamefanyiwa uthamini na Serikali.
Aidha Wananchi hao wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Tarime
Nyambari Chcha Mariba Nyangwene walisema hayo jana
kwenye kikao chapamoja ambacho kiliwajumuisha viongozi wa vijiji hivyo kuwa
wameondoa tofauti zao katika kudai swala zima la Fidia ya maeneo yao ambayo
yamefanyiwa tathimini na serikali.
Akiongea Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mkoa
Mara Nansy Msafiri katika kikao hicho ambacho kilikalia katika ukumbi wa
halmashauri ya Wilaya Tarime,julai,30, 2014 alisema kuwa kunahaja Wananchi
kuunganisha nguvu ya pamoja katika swalazima
la kudai haki ya fidia katika maeneo ambayo yamefanyiwa Uthamini na Serikali
tayari kwa shuguli za Mgodi.
Aidha Msafiri aliongezaa kuwa kuna haja Mgodi kilipan fidia
watu ambao wanaishi karibi na maenewo ya machimbo ambao wamo ndani ya umbali wa
mita 200 na kuwa watu hao wanaadhirika na vumbi ikiwemo na matetemeko ya
Baruti.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya Tarime Amosi Sagara
alisema kupitia kamati ya kikosi kazi kilichoundwa na Wizara ya Ardhi
halmashauri ilishinikiza Mgodi kilipa Fidia Wananchi.
‘’lmashauri ilishinikiza Mgodi kulipa fidia wananchi maeneo
ambayo yamefanyiwa tadhimini na kikosi kazi ambapo Mgodi umelipa fidia Wananchi
katika maeneo ya Nyakunguru,Kewanja,Nyangoto kwa awamu sita’’alisema Sagara.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya alisema kuwa Mgodi unatakiwa
kulipa fidia wananchi ambao tayari wamefanyiwa Uthamini na wale ambao wako
jirani na maeneo ya mcchimbo mita 200 ambapo hayo yapo kisheria.
‘’Wananchi tunahitaji kudai fidia kisheria na bila kushikana
miguu na tuunganishe nguvu pamoja katika swala zima la kudai haki ya fidia
maeneo ambayo yamefanyiwa uthamini sanjari na wale ambao wanaishi ndani ya mita
200 aidha kuna baadhi ya viongozi wachache ambao wanadai wananchi kitu kidogo endapo
watakuwa jambo linapaswa kukemewa’’alisema Henjewele.
Kwa Upande wake Diwani viti
maalumu katika kata ya Matongo Tarafa Ingwe Bi: Philomena Tontora
alisema kuwaTangu mwaka 1982 wataalamu walifanya utafiti na kugundua kuwaeneo
la nyamongo kuna pango refu linaloelekea Misiri pamoja na Mto unaoelekea Mto Tanganyika
ndapo
Mgodi ukianzakuchimba kupita chini ya Ardhi maisha ya Wananchi yatakuwa salama hivyo serikali
iliangalie hilo
mara moja ili kunusuru wananchi hao.
Naye Mbunge wajimbo la Tarime Nyambari Nyangwine katika kikao hicho ambacha alikuwa Mwenyekiti
alisema kuwa wananchi washirikiane na kuungana kwa pamoja kwa lengo la kupata
haki zao.
“Tutaandamana kisheria ili kuweza kupata haki zetu sisi wana
pia natoa agizo kwa Watendaji wa Vijiji,na Kata kuandaa kikao ili kuleta maoni
ya wananchi kwa lengo la kuyawasilisha serikalini”alisema Nyambari.
…..Mwisho…