Nyabigena yanufaisha vijana.
Nyabigena ni Ushirika
uanaounganisha vijana kutoka katika vijiji saba vinavyozunguka mgodi wa dhahabu
wa Nyamongo African Barrick Gold Mine (ABG).
Ushirika huo umeweza kupata
tenda mbalimbali katika mgodi wa dhahabu wa Nyamongo kama vile kufagia ndani ya
mgodi, kukusanya vyuma chakavu, na kupulizia dawa ya ukoko kwa ajili ya kuua
mazalia ya ili kutokomeza maralia.
Kupitia kazi hizo vijana
mbalimbali kutoka katika vijiji saba vinavyozunguka mgodi huo wameweza kupata
ajila za moja kwa moja kupitia ushirika huo wa Nyabigena.
Kirigiti Sasi ni katibu wa
ushirika huo alisema kuwa ushirika huo una jumla ya wafanyakazi 917 ambao wameweza kupata ajila kupitia Miradi
mbalimbali inaoendeshwa na Ushirika huo wa Nyabigena huku Ushirika wa Saccos ukiwa na Wafanyakazi,
122, 300 walinzi na140 wakifanya kazi mbalimbali kupitia uhirika huo na 80 ni
wafanyakazi wa viwanda vidogo vidogo Sido.
“Kupitia Barrick ushirika
wetu umeweza kuanzisha miradi mbalimbali na kuajili kila rika na vija tumeweza
kuwapa kipaumbele” alisema Kiriiti.
Hata hivyo katibu wa ushirika
huo aliongeza kuwa Licha ya kuwa na
ushirika huo kuwapa vijana vipaumbele katika ajila wameweza kuunda pia ushirika
wa kuweka na kukopa ili kuweza kuwakopesha wanachama wake huku wakisaidia
watoto wanaoishi katika mazinigira hatarishi na Walemavu.
“Watoto wasiojiweza
tunawasaidia kuwalipia karo ili kudumisha mhusiano yetu na wananchi kutoka
katika vijiji saba vinavyozunuka modi wetu” alisema katibu.
…..Mwisho….